Moja kati ya mwananchi (hayupo kwenye picha) akipima maralia kwenye viwanja vya Nyankumbu Mjini Geita. |
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akiwakabidhi baadhi ya akina mama vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu vinavyotolewa bure na serikali kwa wananchi. |
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye maadhimisho hayo. |
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita akiwasilisha salamu zake kwenye maadhimisho hayo. |
NA,JOEL MADUKA,(MADUKA ONLINE)
Ikiwa ni
siku mbili zimepita tangu kuadhimisha
siku ya Malaria Mkoa wa Geita maambukizi
ya ugonjwa huo yameshuka kutoka
asilimia 38.1 mwaka 2015/17 hadi asilimia 17 mwaka 2017/18 kwa mjibu wa takwimu
za Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS).
Aidha
takwimu hizo kitaifa zinaonyesha kwamba maambukizi ya ugonjwa wa Malaria
yameshuka kutoka wastani wa asilimia 14 mwaka 2015/16 hadi asilimia 7.3 mwaka
2017/18.
Akizungumza
na wananchi kwenye viwanja vya Nyankumbu Mjini Geita wakati wa utoaji wa elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa
Malaria Mkuu wa
Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema mafanikio hayo ni matokeo ya kazi
nzuri ya serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kuondoa vifo vinavyotokana
na Malaria ambapo takwimu zinaonyesha kwamba wastani wa mtu mmoja hupoteza
maisha kila baada ya dakika moja kutokana na ugonjwa huo unaoambukizwa na mbu
jike aina ya “Anopheles”.
Ameongeza
kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali wa afya inaendelea na mapambano dhidi ya Malaria ambapo mwaka jana
ilitoa lita 8,380 za dawa ya viua dudu katika mazalia ya mbu pamoja na kugawa
bure vyandarua vyenye dawa kwa wananchi.
Mganga Mkuu
mkoani Geita, Dr.Japhet Simeo Amebainisha kwamba mkoa wa Geita unasumbuliwa na
maambukizi ya Malaria kutokana na sababu za kimazingira ambapo kuna nyuzi joto
18 hadi 32 linalochochea uendelevu wa mbu hivyo ni vyema wananchi wakahakikisha
wanatunza vyema mazingira yao ikiwemo kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ili
kuangamiza mazalia ya mbu.
Wananchi na
wanafunzi mkoani Geita waliitikia vyema zoezi la upimaji Malaria na utoaji bure
dawa kwa waliobainika kuwa na ugonjwa huo .
Post A Comment: