Kamanda wa Polisi Mkoani Geita,Mponjoli Mwabulambo akithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Erick mkazi wa Mtaa wa
14 Kambarage Kata ya Buhalahala wilayani Geita ameuawa kisha mwili wake
kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kuvunja Duka la Bw Michael
Yusuf na kuiba Sh elfu ishirini(20,000) .
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wananchi kumtuhumu kijana huyo
kujihusisha na uhalifu wa mara kwa mara na kwamba kipindi cha nyuma amewahi
kuhusika na ubakaji wa Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini (60).
Baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio wamesema kijana
huyo amekuwa na kawaida ya kufanya uhalifu kwenye maeneo mbalimbali kabla ya
kuuawa.
“Tunasikitika sana na tabia ya baadhi ya vijana kushindwa
kufanya shughuli kwa njia ya harari na kujipatia kipato matokeo yake wamekuwa
wakitumia njia za panya kutafuta mafanikio ya haraka jambo ambalo sio sahihi
kabisa mimi nisema hatua ambayo wameichukua wananchi sio nzuri ni bora
wangeacha nyombo vya usalama vitatue tatizo hili”Alisema Bi,Jamila Hassani.
Baadhi ya wazee wa mtaa huo wamesema vijana wanaojihusisha
na uhalifu wamekuwa wakihifadhiwa na mmoja wa wananchi wa eneo hilo .
“Hapa mtaani kuna mkubwa wao ambaye amekuwa akiwatunza
vijana hawa ingawa tunamjua ila hatutaki kumsema tumemuhifadhi siku nyingine
tutamtaja endapo akiendelea na tabia hizi sisi wazee zinatuchukiza sana”Alisema
Mzee Safari Malando.
Mwenyekiti wa mtaa huo Bw,Mfaume Nkerebe amesema anamfahamu
marehemu kutokana na vitendo vyake vya uharifu na kwamba tukio hilo sio la kwanza
kwani alishawai kuiba kwenye stational na kumbaka bibi kizee wa miaka sitini.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Bw Mponjoli Mwabulambo
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwataka wananchi kutokujichukulia
sheria mkononi.
|
Post A Comment: