Baadhi ya wanavikundi vya ujasiriamali wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Geita.
Halmashauri
ya Wilaya ya Geita imetoa kiasi cha Sh,Milioni 173.5 ikiwa ni mwendelezo wa
halmashauri kuhakikisha asilimia 10% ya makusanyo ya ndani inatolewa kwa
vikundi vya wanawake ,vijana na walemavu ili kuweza kuvisaidia kujinyanyua
kiuchumi kupitia shughuli ambazo wamekuwa wakizifanya za ujasiriamali.
Katika azima
ya kuwawezesha wananchi,hususani wanawake,vijana na walemavu halmashauri hiyo
imeendelea pia kutoa elimu na kufanya uhamasishaji katika kata 37 kwa lengo la
kuhimiza wananchi kujiunga kwenye vikundi vya ushirika na kuchangiana mitaji
yao wenyewe ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi midogo midogo ya kujiongezea
kipato.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw,Ali Kidwaka ametaja changamoto ambazo wamekuwa
wakikutana nazo ni pamoja na wakopaji kutokuwa na utayari wa kurejesha feza
hizo kwa wakati na wanakikundi kuhama kutoa eneo moja kwenda jingine bila ya
kutoa taarifa.
Aidha kwa
upande waka Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amewasisitiza wajasilia
mali hao kutokuwa na uwoga wa kukopa na pia kuzitumia fedha hizo kwenye
matumizi sahihi ya kujikwamua kimaisha.
Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo Elisha Lupuga amewasisitiza wanavikundi ambao wamepatiwa
mkopo huo kutokutumia kinyume na makubaliano ambayo yamepangwa na serikali bali
wafanyie shughuli ambazo zitawasaidia kuinua vipato vyao.
Mkuu wa Mkoa
Huo,Mhandisi Robert Gabriel ameziomba taasisi za kifedha kuendelea kutoa elimu
ya utunzaji wa fedha.
Baadhi ya
wanavikundi ambao wamepatiwa fedha hizo wameishukuru serikali kwa namna ambavyo
imeendelea kujitoa kuwasaidia wananchi ambao wanamaisha ya chini.
|
Post A Comment: