NMB YAFUNGUA MATAWI MAWILI MWANZA

Share it:
Afisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB,Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la NMB-Igoma Mwanza.



Meneja wa Kanda ya ziwa wa NMB ,Bw Abraham Augustino akiwatambulisha baadhi ya watumishi wa NMB wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tawi la NMB Igoma.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza(Kulia)John Mongela akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana wakati wa shughuli ya uzinduzi wa Tawi la NMB Igoma.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza(Katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NMB.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza(Kulia)John Mongela akifurahia na Afisa biashara wa NMB Bw,Abdulmajid Nsekela baada ya kuzindua tawi la Igoma.
Katika kuhakikisha kuwa inatambua mchango wa wananchi ambao wamekuwa wakitumia huduma za Kibenki,NMB Benki wamekuwaja na huduma ya mikopo ambayo inawahusu wananchi wa kipato cha chini ambayo itawasaidia kuinua uchumi wa biashara ndogo ambazo wamekuwa wakizifanya.

Akizungumza na wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye shughuli ya ufunguaji wa tawi jipya la Igoma Jijini Mwanza ,Afisa Mkuu wa Biashara wa NMB,Bw Abdulmajid Nsekela,amesema kuwa  wameendelea kutumia kauli mbiu ya karibu yako kwa maana kuwa karibu na mteja kwa kutoa huduma za kibenki ,kumshauri mteja kupata huduma hizo na kutengeneza bidhaa nzuri ili kupata mlaji kulingana na mahitaji tofauti tofauti ya wateja.

Aidha ameongezea kuwa hadi sasa Benki hiyo inamawakala 5000 na kwa mkoa wa mwanza Pekee inamawakala takribani 200 na kwa igoma wapo saba ingawa kumekuwepo na orodha ndefu ya baadhi ya wafanyabiashara kuomba kuwa mawakala.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela amesema kuwa serikali inatambua na kutoa kipaumbele katika kuendeleza sekta ya Benki nchini.

Na kwamba anatambua kuwa kazi hiyo ya kuwahudumia wananchi ni jambo nzuri na la busara ikiwa ni pamoja na kuendelea kujitolea vifaa mbali mbali kwenye ngazi ya afya  na sekta ya elimu.


Share it:

BIASHARA

Post A Comment: