Mkulima wa mpunga kutoka kijiji cha Nyawilimelwa Bw Lazaro Lujina akizungumza juu ya hataua ya wao kuendelea kuhuza mazao yao kwa bei ya hasara. |
Baadhi ya magunia ya Mpunga yakiwa kwenye ghara la kuhifadhia mazao hayo. |
Bw Rashid Kibashala akizungumza juu ya hatua ya kuendelea kununua kwa bei za chini na wao kuhuza bei ya Juu. |
Ngunia ambalo wakulima wamekuwa wakililalamikia kuwa limekuwa likiwasababishia hasara kutokana na ujazo wake ulivyo. |
Wakulima wa Mpunga kijiji cha Nyawilimelwa Wilayani Geita
Mkoani humo wameiomba Serikali kuwatengenezea Soko la pamoja ambalo litasaidia
kuuza mazao yao kwa bei nzuri zaidi kuliko sasa hivi ambavyo wamekuwa wakiuza
bei ya hasara kwa walanguzi wanaoingia kijijini Humo.
Wakizungumza mtandao huu Kijijini hapo baadhi ya wakulima
wamesema kukosekana kwa soko nzuri la kuhuzia mazao yao imekuwa ni sababu ya
wao kuhuza kwa bei isiyo nzuri na pindi
wanapotaka kupereka mjini wamekuwa wakikutana na changamoto ya ubovu wa
Barabara.
“Tatizo ni kukosekana kwa soko ndio sababu ambayo imekuwa
ikisababisha sisi wakulima kushindwa kukaa na mazao kwa muda mrefu ndani na
unakuta na sisi tunashida nadhani serikali ingeona umuhimu ikatutengenezea soko
ingependeza zaidi kama vile pamba tunaona inasoko lakini mpunga hauna soko
kabisa”Alisema Julius Mandegere.
Kutokana na malalamiko ya wakulima kunyonywa na baadhi ya
walanguzi mtandao imezungumza na Mlanguzi wa mazao hayo,Bw Rashid Kibashala ambapo amesema mala nyingi wamekuwa wakifanya
maelewano kabla ya biashara.
“Kila biashara inamaelewano hivyo sisi tunafanya maelewano
na wakulima juu ya bidhaa ambayo tunanunua kwa lengo la kwenda kupata faida
siunajua kaka na sisi tunasafirisha hivyo tunaitaji faida sisi hatuwanyonyi”Alisema
Kibashala.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho,Bw Majuto Mariatabu amesema hili
kuwasaidia wakulima kutokuuza mazao yao holela wamekuwa wakiwakamata wale ambao
wameendelea kuwagalaliza wakulima hao.
Afisa Kilimo wa Mji
wa Geita,Bw Samweli Ng’wandu akielezea
namna ambavyo wametoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa utunzaji wa chakula
hususani katika kipindi hiki cha mavuno.
Post A Comment: