MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU WAPATA AJALI

Share it:

Majeruhi wakipatiwa huduma ya kwanza.


Gari likiwa limepindukia kichakani 

Watu 4 wamejeruhiwa katika msafara wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya gari moja kuanguka huko Nanguruwe wakati wakitoka Mtwara kuelekea Tandahimba.

Inaelezwa kuwa msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais Mtwara.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara.

Habari zinasema kuwa majeruhi katika ajali hiyo ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais na wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa Channel ten, Star Tv na Clouds Tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba siyo ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.

Share it:

matukio

Post A Comment: