Hudson Kamoga akiwa kwenye majukumu ya kila siku. |
Horodha ya uteuzi. |
Rais John Magufuli
leoamemteua Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na
uteuzi huu umeanza leo.
Imeeleza kuwa Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa
jana ambao ni Ado Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na
Tixon Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa
katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli
amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mji mmoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa moja ili kujaza nafasi
zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo Godwin
Kunambi(Manispaa ya Dodoma), Elias Ntiruhungwa(Mji wa Tarime), Mwantumu
Dau( Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba), Frank Bahati(Halmashauri ya Wilaya ya
Ukerewe), Hudson Kamoga(Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu), Mwailwa
Pangani(Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo).
Wengine ni Godfrey Sanga(Halmashauri ya Wilaya ya
Mkalama), Yusuf Semuguruka(Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga), Bakari
Mohamed(Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea), Juma
Mnwele(Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo), Butamo Ndalahwa(Halmashauri ya Wilaya
ya Moshi), Waziri Mourice( Halmashauri ya Wilaya ya Karatu) na
Fatma Latu( Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo)
Post A Comment: