Na Makunga Makunga
MAHAKAMA ya Mwanzo ya Masumbwe Wilayani Mbogwe imemuhukumu
kifungo jera miezi 36 na kuchapwa viboko 24 matakoni Mganga wa Jadi (Sangoma ) Sabas Majaliwa
(42)mfipa mkazi wa Mwanza baada ya
kumtapeli mlemavu wa miguu Paul Mpangabule
kwamba atamtengenezea fedha za utajiri kwa njia ya majini .
Hakimu wa mahakama
hiyo ya mwanzo masumbwe mh Sunga
Emmanuel Mechara amesema kifungu
cha 32 cha kanuni za mwenendo wa mashauri ya jinai katika mahakama za mwanzo
ambayo ni nyongeza ya tatu ya Sheria ya
mahakama za mahakimu sura ya 11 iliyofanyiwa mapitio 2002.
amemuhukumu Sabas Majaliwa kwa kosa la kujipatia Fedha kwa
njia ya udanganyifu kinyume na kifungu cha 302 sura ya 16 kanuni ya adhabu.
Mh Mechara amesema Sabas Majaliwa ametiwa hatiani baada ya
kukiri shitaka aliloshtakiwa nalo na amepewa adhabu ya kifungo jera miaka 3
sawa na mizi 36 pamoja na kuchapwa viboko 24 matakoni baada ya kupimwa na
daktari ili iwe fundisho kwa waganga wengine wa jadi wanaendesha mchezo huo wa
utaperi wa kuwatengenezea fedha za majini ili watajirike.
Mahakamani hapo ilidaiwa kuwa majaliwa siku ya agosti 20
mwaka huu alimtapeli sh. 435,000 Paul Mpangabule 53 mlemavu wa miguu yaani
kiwete mkazi wa mtaa wa shy A nyakafuru
akiwa yeye na mke wake watengenezewe fedha za utajiri za majini,ili
watajirike.
Mganga huyo baada ya kuchukuwa fedha sh 435,000 alifika
na vitambaa viwili cheupe na chekundu
chungu kidogo ,udi na ubani na sanduku
kubwa litakalojazwa fedha na chupa
aliyodai inamafuta ya Binadamu ambayo
yalipakwa kwenye fedha hizo wakainamishwa kwenye sanduku na kuogeshwa
fedha baada ya hapo mganga akatoweka na fedha hizo akidai anazipeleka
makaburini kufanya tambiko .
Aliporudi mganga akawaomba sh. Milioni tatu ili
wazichanganye na fedha za majini
watakatishe fedha hizo na zile za jasho lao wakakosa akawaambia wakakope
ili wazilete waanze kuhesabu ndipo walipopata ufahamu na hatimaye askari polisi
kituo cha masumbwe wakamkamata na kumfikisha mahakamani.
Mshitakiwa majaliwa ameomba apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mke ,watoto na mama yake
mjane anaowatunza na wanamtegemea.
Post A Comment: