Waangalizi wa uchaguzi wa wabunge wa Shelisheli katika picha
ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Dk. Augustine Mahiga na Balozi Innocent Shiyo. (Picha kwa hisani ya Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Tanzania ilikabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa kuongoza Asasi
ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC
Organ), katika Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika huko
Mbabane, Swaziland tarehe 29 – 31 Agosti, 2016.
Mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Mheshimiwa Dkt.
Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki alielekea Jamhuri ya Shelisheli kwa lengo la kumwakilisha Mheshimiwa
Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuongoza
ujumbe wa Waangalizi wa SADC katika Uchaguzi wa Shelisheli utaofanyika tarehe 8
- 10 Septemba, 2016.
Wajibu huu wa Tanzania katika kuongoza misheni hiyo ya
waangalizi wa uchaguzi imetokana na misingi na muongozo wa chaguzi za
kidemokrasia katika Kanda ya SADC. Akiwa nchini Shelisheli, Mheshiwa Mahiga
(Mb), alizindua rasmi misheni hiyo
tarehe 2 Septemba, 2016 kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Magufuli. Misheni hiyo ya
waangalizi itakua na waangalizi kutoka nchi
za SADC .
Wakati akiwa nchIni Shelisheli, Mheshimiwa Waziri Mahiga
alipata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mhe. James Alix Michel Rais wa Sheliseli .
Pia Mheshimia Waziri
Mahiga aliweza kufanya mazungumzo na Mhe. Joel Morgan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Seychels na
kukutana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi ya Seychels.
Imetolewa na :
BALOZI INNOCENT E.
SHIYO
|
Post A Comment: