Timu ya Brazil imeitwanga Argentina ya
Lionel Messi jumla ya magoli 3-0 katika michuano ya kuwania kufuzu kombe
la Dunia itakayochezwa nchini Urusi mwaka 2018.
Brazil walianza kuliona lango la akina
Messi dakika ya 24 Philipo Countinho aliwanyanyua washabiki kwa goli
safi akipokea pasi toka Neymar kabla timu hazijaenda mapumziko Neymar
alifunga goli la pili mnomo dakika ya 45 hadi mapumziko wenyeji walikuwa
mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa Argentina
kujaribu kutafuta angalau hata goli walishindwa kupita ukuta wa wenyeji
katika dakika ya 59 kiungo wa zamani wa Tottenham Spurs kwa sasa
anacheza soka nchini China Paulinho alifunga goli la tatu na kupeleka
kilio kwa mashabiki wa Argentina hadi mwamuzi wa mchezo huo anapuliza
kipenga cha mwisho Brazil wameibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Kwa matokeo hayo Brazil wameendelea
kubaki kileleni wakiwa na pointi 24 wakati Argentina wameshuka hadi
nafasi ya sita wakiwa na pointi 16 ya msimamo wa hatua ya kufuzu kombe
la Dunia 2018.
VIKOSI:Brazil: Alisson;
Alves, Miranda (Silva 87), Marquinhos, Marcelo; Fernandinho, Paulinho,
Renato Augusto; Coutinho (Costa 84), Neymar, Gabriel Jesus (Firminho 82)
Goals: Countinho 24, Neymar 45, Paulinho 59
Yellow cards: Fernandinho, Marcelo
Argentina: Romero; Zabaleta, Otamendi, Funes Mori, Mas; Perez (Aguero 46), Biglia, Mascherano, Di Maria (Correa 71); Messi, Higuain
Post A Comment: