DC KASESELA : WANANCHI WATAKIWA KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA

Share it:

IMG_20170406_123026
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo
 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard 
Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na 
kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua 
mikononi.
 
Ameyasema hayo baada ya 
kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya 
kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na 
kutelekeza kiliwili chake.
 
“Kwanini watu wajichukulie 
hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti 
huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote 
na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa
tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela
 
Kasesela alisema kama wilaya 
wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia 
sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la 
polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.
 
“Wilaya ya Iringa ilikuwa 
imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye 
uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na 
lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina 
kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela 
 
Kasesela ameeleza kuwa tukio 
hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani 
nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.
 
Aidha Kasesela amewaomba 
viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya 
kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi.

Na Fredy Mgunda,Iringa
 

Share it:

JOEL MADUKA

habari

Post A Comment:

Also Read

MILIONI 173.5 ZATOLEWA KWENYE VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WALEMAVU GEITA

Mkuu wa mkoa mhandisi Robert Gabriel akikabidhi hundi ya fedha kwa Mwenyekiti wa kikundi cha walemavu cha Ludete Bw,Ju

JOEL MADUKA