Kuna tofauti kubwa sana iliyopo kati ya kazi na ajira, unashaanga ndo ukweli huo. Tulio wengi huwa tunazama kazi kama ajira kumbe ni vitu viwili tofauti. katika makala yetu ya leo tutakwenda kuangalia tofauti hizo kati ya ajira na kazi na thamani ya kufanya kazi.
Tukianza na kujua maana ya Kazi, kazi ni shughuli yeyote ile iliyo halali au isiyo halali ambayo huifanya mtu kutokana na ujuzi, kibaji na ubunifu ili kupata mapato na faida, ila katika mafanikio tunazungumzia kazi halali tu.
Ila ajira ni kile kitendo cha kuuza muda,ujuzi, ubunifu na kumtumikia mwingine, hii hutokea kwa kuwa wewe hujaamua kufanya kazi ya mwenyewe ila umeamua kuajiriwa. Daima tukumbuke ya kuwa kazi ndiyo ambayo inayoanza kabla ya ajira . Ajira ni mizizi ya utumwa nasema hivi nikiwa nina maana ya kwamba kwa kuwa hii karne ya ishiri na moja baadala ya kuwaita watumwa basi wanaitwa wafanyakazi.
Leo ingekuwa ni tarehe moja mwezi wa nne ungesema Afisa anaongopa, sijaongopa na huo ndio ukweli usiopingika. kuna baadhi ya watu wao huamini ya kwamba bila ajira wao hawawezi kuishi jambo hilo halina ukweli wowote ndani yake. Sina maana ya kusema eti kuajiliwa ni kubaya hapana, ila ukweli ni kwamba ni lazima ufikiri nje box, yaani kitu kingine zaidi ya kutengemea kulipwa mshahara ila ifike mahali na wewe ulipe watu mshahara.
Watu wengi waliojiriwa wanasema Mwenyezi Mungu ibariki kazi ya Mikono yangu, Je Hiyo ni Kazi ya mikono yako au ya mwajiri wako? Ukitaka kusema hayo azisha kitu chako harafu ndo useme Mwenyezi Mungu bariki kazi ya mikono yangu na baraka zitakuja kweli. Daima tukumbuke ya kuwa binadamu ameubwa ili kufanya kazi, ukisema wewe ni mcha Mungu ni lazima ufanye kazi. Ukisoma katika Vitabu vya Dini vinatufundisha ya kuwa, siku zote baraka za kiuchumi zinapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii.
Pia mpango wa Mungu kwa watu wake baada ya kuwaumba ilikuwa ni watu hao kwenda kuitawala nchi na sio watu. Kutawala nchi kwa maana ya kuwa kuitazama nchi na vitu vilivyoko ndani yake katika uzalishaji kama vile ardhi katika kufanya kazi za usalishaji. Kuna kitabu fulani cha kimafanikio kiliandikwa ya kwamba hapa duniani kuna kila aina ya kitu ambacho mwanadamu akikitumia vizuri atakuwa tajiri.
Ila tatizo kubwa ni kwamba watu waliopo ndani yake hawavitumii vitu hivyo. Swali la kujiuliza je vitu hivyo Mungu alivyotupa vinakupa manufaa gani au ndio unazidi kulaumu kwa kusema maisha ni magumu? ukweli ni kwamba tumia vitu vilivyopo ili kupata mafanikio makubwa.
Thamani ya kufanya kazi ni kama ifuatavyo;
1. Thammani za kufanya kazi huja kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidiii siku zote. Muda muafaka wa wewe kuamuamua kufanya kazi ndo huu sasa. Unapenda kuendelea kuita boss maisha yako yote au kuitwa boss, usinipe jibu. ila kumbuka kila ya siku ili kukata kiu yako ya mafanikio kunywa kinywaji kinachoitwa bosi, ukifanya hivyo kweli utakuwa bosi.
2. Ubunifu.
Thamani ya kufanya kazi huja kwa mtu kuwa mbunifu, Ubunifu huanza kwenye wazo jipya, wazo ndio chanzo kikubwa na ndio siri kubwa iliyojificha kuapata atajiri. Siku zote ukumbuke ya kuwa ni mtu mwenye mawazo mapya yenye kuleta mafanikio makubwa mbele yako. Kuwa mbunifu ili umiliki kazi yako ili uweze na wewe kuitwa bosi maana inawezekana kabisa.
Navigation
Post A Comment: