Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu, viongozi na wadau wa tiba Asili na tiba Mbadala wakati wa uzinduzi wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala uliofanyika leo katika viunga vya ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Shastri Herbals Namdeo Shastri akionesha cheti cha usajili alichopewa leo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala uliofanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa kampuni yakimataifa ya Cornwell Quality Tool & Chemicals Bi. Elizabeth Lema akipokea cheti cha usajili cha Tiba Asilia na Tiba Mbadala kutoka kwa Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala.
Wadau wa tiba Asili na tiba Mbadala wakifuatilia kwa umakini hotuba ya uzinduzi wa mpango mkakati wa Tiba asili na Tiba mbadala uliofanywa na Mh. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango mkakati wa Tiba asili na Tiba mbadala, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Wizara ya Afya Dkt. Edmund Kayombo, kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Otilia Gowele na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Tiba asili na Tiba Mbadala Dkt. Muhame.
Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala, Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Otilia Gowele na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Wizara ya Afya Dkt. Edmund Kayombo.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepiga marufuku watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kutangaza dawa za asili ambazo hazijasajiliwa na Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala kisheria.
Hayo amezungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa tiba asili na tiba mbadala ili kuweza kuwaongoza watoa huduma za tiba asili kuweza kutoa huduma bora na salama kwa watanzania wanaotumia tiba hizo.
“Dawa zote za asili zinazotengenezwa na watoa huduma za asili lazima zisajiliwe na baraza husika kwa mujibu wa sheria ili kupata usalama wa matumizi kwa watanzania na marufuku kwa watoa huduma wa tiba asili kutangaza dawa hizo kama hazijasajiliwa” alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala wanawajibu wa kuwa na sehemu maalum ya kutengenezea dawa zao na mahali pakutolea huduma zao ili kutowachanganya wateja wao wanapohitaji tiba asilia.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa pindi watoa huduma ya tiba asili na tiba mbadala wanaposajili dawa zao zitaongeza chachu ya kutengeneza viwanda vya dawa hizo ili kusapoti juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Wizara ya Afya Dkt. Edmund Kayombo amesema kuwa dawa za tiba asili zinatakiwa kusajiliwa ili kuweza kutambua na kuweka usalama kwa watumiaji wa dawa hizo.
Aidha Dkt. Kayombo amesema kuwa umuhimu wa kusajili dawa hizo ni kuwasaidia watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kuweza kupata soko kimataifa na kutangaza bidhaa za Tanzania nchi za nje ili kuongeza ushindani wa biashara.
Kwa upande wake mtoa huduma za tiba asili na tiba mbadala Bi. Elizabeth Lema amesema kuwa wanapaswa kusajili dawa zao ili kuwathibitishia ubora na usalama watumiaji wa dawa za tiba asili na tiba mbadala nchini.
Post A Comment: