WADAU WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTOKOMEZA NA UKATILI WA KIJINSIA.

Share it:
Mkurugenzi wa Kawiye Social Development Foundation (KASODEFO) Ezekiel Kasanga akiongea na wadau wa maendeleo wilayani Itilima mkoani Simiyu namna ya kupambana na ukatili wa kijinsia ambao bado umeshamili wilayani humo.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima Dr Kesam Maswagwa aliyeshiriki katika semina hiyo na kusema kuwa ukatili wa kijinsia hukwamisha maendeleo ya kaya na kuzifanya kuwa duni.


Wadau wa maendeleo wanaopinga ukatili wa kijinsia wilayani Itilima.

Nyansato Mahungururo afisa Maendeleo ya jamii Itilima aliyeshiriki zoezi hilo       
Na COSTANTINE MATHIAS, Itilima.

WADAU wa Maendeleo nchini wametakiwa kujikita katika kukomesha ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ili kuwa na taifa huru kuelekea uchumi wa viwanda kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.

Wilaya ya itilima mkoani Simiyu bado inakabiliwa na tatizo hilo ambapo matukio hayo yamekuwa hayaripotiwi katika vyombo vya dola huku  katika mpango wa taifa wa serikali wa mwaka 2017/2022 unaonyesha kuwa wanawake wanne kati ya 10 wanafanyiwa ukatili hasa wa kingono.

Akiongea na wadau wa maendeleo wilayani humo Mkurugenzi wa Kawiye Social Development Foundation (KASODEFO) Ezekiel Kasanga alisema kuwa tatizo la ukatili wa kijinsia bado lipo katika maeneo mengi nchini na kuwataka wadau hao kuhakikisha wanapiga vita aina zote za ukatili.

Alisema kuwa dhamira kuu ya jumuiko hilo ilikuwa ni kukutana kama  wadau na kutengeza mtandao wa pamoja ili kudhibiti ukatili wa kijinsia  dhidi ya wanawake na watoto huku akitaja kuwa wilaya ya Itilima bado inakabiliwa na tatizo hilo.

‘’kimsingi tatizo la ukatili katika wilaya ya itilima bado lipo, katika takwimu za mpango wa serikali kwa mwaka 2017 hadi 2022, serikali inatumbia kuwa kati ya wanawake kumi wanne kati yao wanafanyiwa ukatili hasa wa kingono..tunaielimsha jamii kuachana mila na desturi potofu zinazopelekea I ya wanawake.’’ Alisema Kasanga.

Aliitaka jamii kupokea elimu ili wapate maarifa juu ya ukatili wa kijinsia na pia washirikiane na vyombo vya serikali katika kuwafichua na kuchukua hatua kwa wanaofanya ukatili ili kuwa na jamii yenye usawa.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima Dr. Kesam Maswagwa alisema kuwa kwa upande wa serikali matatizo ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ni kikwazo kwa maendeleo ya familia kwa sababu kaya nyingi zinapofanyiwa ukatili zinaendelea kuwa duni na kusababisha hata ukuaji wa maendelea kwa taifa unakuwa duni vilevile.

Maswagwa alisema kuwa ukatili wa kijinsia ni kikwazo kwa maendeleo kwa sababu kaya nyingi zinazofanyiwa ukatili huo zinakuwa duni na zinaendelea na uduni,hivyo wadau wajitahidi kushiriki katika mpango mkakati wa serikali wa kupiga vita ukatili wa kijinsia ifikapo 2022.

Nao wadau wanaojihusisha na ukatili wa kijinsia ambao walishiriki katika semina hiyo wanasema kuwaukatili mwingi huanzia majumbani na hufanywa na ndugu wa karibu, hivyo ni vyema wadau wakashirikiana kuwajengea uelewa wananchi juu ya kuripoti aina zote za ukatili unaojitokeza katika maeneo yao.

‘’naomba muwashauri kama mtu amepigwa, kaumizwa  iliwaende polisi kuchukua poilisi pia mtuhumiwa akamatwe, ili tushirikiane kupambana na uhalifu wa aina yeyote ile,..sisi ndiyo tunakaa na jamii na jamii nyingi inayoishi vijijini bado inaabudu mila ambazo ni za kikatili na wananshindwa kuzilipoti mahali husikam kupitia huu muunganiko utatuasidia kutokomeza ukatili’’ alisema Nyansato Mahunguriro amabye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Itilima.

Ukatili mwingi umekuwa ukitokea katika familia kwa kuwahusisha ndugu wa damu na kuwafanya kushindwa kuripoti ngazi husika kwa kuona kuwa wataaibishana  na badala yake mtendewa kubaki na athari za kisaikolojia ikiwemo mimba na kuambikizwa magonjwa ya zinaa.
Share it:

habari

Post A Comment: