NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI
wa
Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (pichani juu), amewaomba radhi wananchi
kufuatia kukatika kwa umeme nchi nzima Oktoba 25 na 26, 2017
kulikosababishwa na hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa.
Dkt.
Kalemani ambye alikuwa mjini Dodoma akishiriki vikao vya kamati za
bunge, alilazimika kusafiri mapema leo asubuhi Oktoba 26, 2017 kuja
jijini Dar es Salaam ili kufuatilia juhudi za kurekebisha tatizo hilo.
"Ndugu
wananchi hali ilivyotokea sisi kama Shirika la TANESCO na Serikali
tunawataka radhi wananchi kwa matatizo yaliyotokea lakini niseme tu
kwamba kuna hatua madhubuti zinazochukuliwa hivi sasa kurekebisha hali
hiyo ili wananchi muendelee kupata umeme wa uhakika." Alisema Dkt.
Kalemani katika taarifa yake kwa wananchi aliyoitoa makao makuu ya
Wizara jijini Dar es Salaam baada ya ziara yake ya kutembelea kituo cha
udhibiti cha Gridi ya Taifa, (GCC), kilichoko Ubungo na kituo cha kufua
umeme wa gesi cha Kinyerezi1 jijini Dar es Salaam.
Taarifa
za awali zilieleza kuwa
kukatika kwa umeme kulisababishwa na "Gridi kuchomoka" Oktoba 25,
2017 majira ya saa 10;08 alfajiri na kurejea saa 12:09 asubuhi ambapo
umeme ulirejea mikoa yote isipokuwa Zanzibar, ingawa juhudi za mafundi
wa TANESCO ziliwezesha umeme kurejea Zanzibar majira ya saa 1 asubuhi.
Hata
hivyo tatizo hilo lilirejea tena majira ya saa 12:30 jioni siku hiyo
hiyo ya Oktoba 25, 2017, ambapo takriban mikoa yote iliathirika. Umeme
ulirejea tena majira ya saa 3 usiku lakiji ilipofika Oktoba 26, 2017
majira ya saa 12:03 tatizo hilo likajirudia tena na kuathiri takriban
mikoa yote ikwiemo Zanzibvar.
"Nimekuja
kutoka Dodoma ili kuona nini kimetokea, nini kimesababisha na hatua
gani za haraka zichukuliwe ili kuondoa tatizo hilo hii ndio hasa dhamira
ya safari yangu." Alisema Dkt. Kalemani baada ya kufika kwenye kituo
cha udhibiti Gridi ya Taifa, Ubungo.
Lakini niwapongeze TANESCO kwa kutoa taarifa mapema kwa wananchi kuwajulisha kuhusu tatizo hilo, alisema.
Akifafanua
zaidi Dkt. Kalemani alisema, chanzo cha tatizo ni pamoja na mfumo
wenyewe (GCC) na bado unafanywiwa marekebisho na taratibu zinaendelea,
na kule Kinyerezi kuna mashine moja haifanyi kazi nayo inafanyiwa
marekebishiom ikiwa ni pamoja na valvu moja iliyoharibika nayo pia
inafabnyiwa kazi.
"Gridi
ya taifa imerejea tangu jana usiku (Oktoba 25), na umeme unapatikana
nchi nzima lakini hata hivyo yapo maeneo machache ambayo hayapati umeme
wa kutosha kwa sababu mtambo mmoja wa Ubungo namba mbili wenye jumla ya
megawati 129 haujaanza kufanya kazi na nimeelekeza wataalamu wafanye
kazi usiku na mchana na wamenihakikishia kufikia saa 5 asubuhi kesho
(Oktoka 27), mtambo huo utaanza kufanya kazi na umeme utarejea katika
hali yake ya kawaida." Alibainisha.
|
Post A Comment: