Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya
matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya
sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya
ya Maswa, Mwl. Joseph Mashauri vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi
la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Na Stella
Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.
Wizara ya Elimu pamoja na
wadau wengine wa Elimu wametoa vitabu 16,985 kwa shule za Sekondari za Mkoa wa
Simiyu kwa ajili ya matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza
na elimu ya sekondari (baseline course).
Akikabidhi vitabu hivyo kwa Maafisa Elimu wa
Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka
amesema vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa Mkoa huo, vikitumiwa vizuri na walimu
wenye nia ya kufanya mapinduzi ya elimu na kuwasaidia wanafunzi kujua maana
halisi ya vitabu hivyo, vitasaidia Mkoa wa Simiyu kufikia malengo ya
kiushindani katika Elimu.
Ameongeza kuwa lengo la
Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata vitabu pamoja na mahitaji
mengine ikiwa ni pamoja na madawati, walimu, vyumba vya madarasa
vinavyotolesheleza hivyo akasisitiza vitabu hivyo vikatumike kwa kusoma ili
viwasaidie.
“Vitabu hivi mtakapogawiwa
mkavitumie kwa ajili ya kusoma visiwe mapambo na kama mwanafunzi hujui uliza,
jibidiishe kujua kitabu hicho kinahusu nini na kama hujaelewa muulize mwalimu
ili kesho kwenye mtihani ufaulu kama wenzako wananvyofaulu” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amewataka
Maafisa Elimu mkoani humo kuzungumza na walimu kabla ya kugawa vitabu hivyo ili
vitakapogawiwa katika shule vigawiwe katika utaratibu mzuri utakowawezesha
walimu kuwasadia wanafunzi kuvitumia kwa manufaa.
Akitoa taarifa juu mapokezi
ya vikao hivyo Katibu Tawala Mkoa amesema Mkoa huo umepokea jumla ya vitabu
16,000 kwa ajili ya wanafunzi na vitabu 985 kwa ajili walimu(kiongozi cha
mwalimu).
Akizungumza kwa niaba ya
Maafisa Elimu Sekondari mkoani humo, Afisa Elimu Sekondari wa Halmahauri
ya Mji Bariadi Mwl. Esthom Makyara amesema vitabu hivyo ni msingi mzuri kwa
wanafunzi wa kidato cha kwanza na Maafisa Elimu hao wanapaswa
kuwaelekezaWakuu wa shule kutofungia vitabu hivyo stoo badala yake
wanafunzi wapewe ili wavisome.
Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa
wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga amesema Maafisa Elimu Sekondari wahakikishe
vitabu hivyo vinagawiwa kwa wakuu wa shule kabla ya shule kufunguliwa Januari
08, 2018, ili wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapoanza masomo wavikute
shuleni.
Baadhi ya wanafunzi wa
kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Bariadi walioshuhudia zoezi la
ugawaji wa vitabu hivyo kimkoa wamesema, vitabu hivyo vitawasaidia wenzao wa
kidato cha kwanza kujenga msingi mzuri wa maarifa ya jumla na lugha ya
Kiingereza.
Vitabu hivi vimetolewa na
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Msaada wa Watu wa
Marekani(UKAID) kupitia Mpango wa Taifa wa Kuinua Ubora wa Elimu hapa nchini
EQUIP-T.
|
Post A Comment: