Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati
akizungumza kwenye kikao cha kazi Mara baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, leo 2
Februari 2018. Picha Zote Na Mathias
Canal
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab R. Telick akitoa taarifa ya sekta
ya madini katika Mkoa huo mbele ya Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka, leo
2 Februari 2018.
Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na
watumishi mbalimbali katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mara baada ya
kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akiwa katika ziara ya kikazi ya
siku mbili mkoani humo, leo 2 Februari 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab R. Telick akitoa taarifa ya sekta ya madini katika Mkoa huo mbele ya Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka, leo 2 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Shinyanga
Naibu Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesifu juhudi
zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainab R. Telack za kukabiliana
na migogoro mbalimbali inayojitokeza jambo ambalo linarahisisha na kuboresha
utendaji wa Wizara ya madini nchini.
Naibu Waziri huyo ametoa pongezi hizo leo 2 Februari 2018 wakati
akizungumza kwenye kikao cha kazi Mara baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa huo wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Shinyanga.
Katika ziara hiyo iliyoanza Leo 2 Februari 2018 na kumalizika
kesho 3 Februari 2018 katika Mkoa wa Shinyanga Naibu Waziri huyo wa wizara ya
madini atatembelea na kuzungumza na wachimbaji wadogo katika eneo la Mwazimba
na Wachimbaji wadogo wa kikundi cha Kasi Mpya.
Mhe Biteko amemweleza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuongeza
msisitizo zaidi katika usimamizi madhubuti wa sheria, Kanuni na taratibu za
nchi pamoja na kuwa na majukumu ya sekta zote lakini sekta ya madini aongeze
juhudi pia ili kuinua mpango wa Wizara ya madini kuongeza nguvu katika mchango kwenye
pato la Taifa kufikia asilimia 10% kutoka asilimia 4% ya sasa.
Naibu Waziri huyo amesema serikali ngazi ya wilaya na Mkoa ni
vema wakaendelea kuwalea wachimbaji wadogo, wakati na wakubwa katika
utekelezaji wa sheria ya madini na kanuni zake.
Aliongeza kuwa Mkuu wa Mkoa na watendaji wote wa sekta ya madini
hawapaswi kuogopa migogoro katika sekta hiyo kwani ili kuwasaidia wachimbaji
wadogo ni lazima kukabiliana na migogoro mbalimbali inayojitokeza baina ya
wachimbaji wenyewe na wawekezaji sambamba na sintofahamu baina yao na baadhi ya
watendaji wa serikali.
Aidha, amekitaka chama cha wachimbaji wadogo nchini kuisaidia
serikali kufichua uovu unaofanywa na baadhi ya wachimbaji Wasio waaminifu ikiwa
ni pamoja na utoroshwaji wa madini mbalimbali jambo ambalo ni kuwaibia
watanzania na kinyume na Sheria ya madini sambamba na usafirishaji wa madini.
Mhe Biteko aliongeza kuwa wachimbaji wadogo na wakubwa kote
nchini wanapaswa kujibainisha katika ulipaji kodi kwani kufanya hivyo
kutaimairisha utendaji wa Wizara katika mchango wa pato la Taifa ikiwa ni
pamoja na serikali kuwatambua na kuongeza ufanisi wa kuwahudumia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa alimweleza Mhe. Biteko serikali ya
Mkoa wa Shinyanga imejipanga kusimamia vema sekta hiyo kwani ni nguzo kubwa ya
uchumia wa Mkoa huo na akaiomba Wizara ya madini kuendeleza ushirikiano na
ofisi yake ili kuongeza tija katika usimamizi wa sekta ya madini.
Post A Comment: