|
Wananchi pamoja na wanasheria wakiwa kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya mahakama ya Mkoa wa Geita. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisalimiana na baadhi ya viongozi wa madhahebu na watumishi wa mahakama wakati alipowasili kwenye viwanja vya maadhimisho ya wiki ya sheria. |
|
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisalimiana na mwanasheria wa kujitegemea Bernad Otieno wakati alipowasili kwenye viwanja vya maadhimisho ya wiki ya sheria. |
|
Wanafunzi wa shule ya msingi Kalangalala wakiimba kwenye maadhimisho ya wiki ya mahakama. |
|
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisaini kitabu cha wageni . |
|
Baadhi ya mawakili wakiwa meza kuu. |
|
Mwanasheria wa serikali Mkoani Geita,Emily Kiria akiwakilisha mada ya faida ya matumizi ya mfumo mpya wa TEHAMA utakavyoweza kusaidia utendaji kazi wa mahakama wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria. |
|
Wananchi pamoja na watumishi wa mahakama wakimsikiliza wakili wa serikali wakati alipokuwa akiwakilisha mada. |
|
Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi mahakama ya Mkoa wa Geita, Ushindi Swalo akijibu baadhi ya mambo ambayo yameelezwa kwenye mada zilizowakilishwa kwenye siku ya maadhimisho ya wiki ya sheria.
|
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkaribisha Mkuu wa mkoa kwaajili ya kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria. |
|
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa mahakama pamoja na kutanguliza nidhamu kwa wananchi ambao wanatakiwa kupatiwa majawabu ya kesi zao. |
Baadhi ya
wilaya za Mbongwe ,Chato,Bukombe na Nyang’hwale Mkoa wa Geita zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa
mahakama za wilaya hali ambayo imekuwa ikisababisha wananchi kwenye
maeneo hayo kutembea umbali mrefu kwaajili ya kwenda kusikiliza kesi zao.
Akizungumza
kwenye viwanja vya mahakama ya Wilaya ya Geita wakati wa maadhimisho ya wiki ya
sheria,Wakili wa serikali Emily Kiria amesema kukosekana kwa mahakama kwenye
wilaya hizo ni chanzo kikubwa cha kusababisha ucheleweshaji wa haki kwa
wananchi.
Hata hivyo
Mkuu wa mkoa wa Geita,mhandisi Robert Luhumbi
ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya sherehe
hizo,ameahaidi kuanza ziara ya kuzunguka kwenye wilaya hizo kuhamasisha ujenzi
wa majengo ya mahakama kwenye wilaya ambazo zinakabiliwa na uhaba.
Wananchi
ambao wapo mjini Geita,Bw Musa Mako na Ally Daniel wamesema mafunzo ya wiki
moja ya sheria kwa wananchi hayawezi kusababisha kuelewa hivyo ni vyema kwa
mahakama kujenga desturi ya kutoa mafunzo hayo mara kwa mara kutokana na kuwepo
kwa tatizo kubwa la uelewa wa sheria na namna ya kuendesha kesi kwa baadhi ya
wananchi.
Wiki ya
sheria imemalizika leo ikiwa ni mwanzo wa shughuli za mahakama kwa mwaka 2018
huku ikiwa na kauli mbiu isemayo” Matumizi ya Tehama katika utoaji wa haki kwa
wakati na kwa kuzingatia maadili”
Post A Comment: