Jafo amwagiza afisa tawala kuunda Tume ya kufatilia ujenzi wa Mradi wa Maji wa kijiji cha Chakorongo Mkoani Geita

Share it:

Naibu waziri wa Tamisemi,Selaman Jafo akizungumza na watumishi wa serikali wilayani Chato Mkoani Geita
Naibu Waziri Wa Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa,Seleman Jafo, Amemwagiza Afisa Tawala Wa Mkoa Wa Geita Kuakikisha Anaunda Timu Maalumi Ya Uchunguzi Ya Kuakikisha Inafatilia Mchakato Mzima Wa Manunuzi Na Majibu Ya Uchunguzi Yapelekwa Kwenye Ofisi Ya Tamisemi Ndani Ya Mwezi Mmoja Na Kwamba Wale Wote Ambao Watakuwa Wamebainika Hatua Kali Za Kisheria Zitachukuliwa.


Hatua Hiyo Imekuja Baada Ya Naibu Waziri Jafo Kufanya Ziara Ya Siku Moja Mkoani Geita,Na Kutembelea Mradi Wa Usambazaji Wa Maji Uliopo Katika Kijiji Cha Chakorongo Jimbo La Busanda Wilayani Geita.

Baada Ya Kujionea Mradi Huo Ambao Umesuasua Kukamilika Kwa Muda Mrefu Na Kusababisha Wananchi Kuendelea Kupata Hadha Ya Maji Katika Maeneo Hayo.Hakuridhishwa Nao Na Ndipo Alipo Hamua Kumwagiza Afisa Tawala Kuunda Timu Ya Uchunguzi Wa Mradi Huo.

Naibu Waziri Wa Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa,Seleman Jafo,Amefanya Ziara Ya Siku Moja Mkoani Geita,Ambapo Ametembelea Mradi Wa Maji Wa Wilaya Ya Chato ,Kiwanda Cha Mafuta Ya Alizeti Pamoja Na Miradi Ya Maji Ya Kijiji Cha Luhuha Na Chakorongo,Pia Amekutana Na Watumishi Wa Serikali Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Chato Na Wilaya Ya Geita Pamoja Na Mji. By Joel Eva Maduka..
Mkuu wa wilaya ya Geita, Herman Kapufi na Naibu waziri wa Tamisemi Seleman Jafo wakikagua mradi wa maji wa Chakorongo.
Mitambo ya kiwanda cha alizeti kilichopo wilayani Chato.
Watumishi wa serikali wakimfatilia kwa makini Naibu waziri wa Tamisemi.
Share it:
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post A Comment: