MASHINDANO YA FARAJI CUP YAMALIZIKA KWA KISHINDO.

Share it:
Mgeni rasimi katika mashindano hayo ambae ni diwani wa kata ya Bukoli,Faraji Rajabu akiwapongeza wachezaji timu ya wakongwe.


Mgeni rasimi akisalimiana na kugagua timu ya Bugogo FC

Akisalimiana na wachezaji wa timu ya Nchimbi FC

Mchezo ukiendelea kwa kishindo katika viwanja vya ccm Bukoli.


Wakifatilia mchezo kwa makini



Mashabiki wakiwa fatilia kwa makini mpambano.

Kombe likiwa linasubilia hatakae linyakua

Mashabiki wakishangilia baada ya ushindi wa nchimbi fc.

Wachezaji wakisubilia maelekezo ya zawadi.


Wakati wa zawadi ukawadia sasa.




Na Joel Maduka Geita.

Michuano Ya Faraji Cup Ambayo Ilikuwa Inaratibiwa Na Diwani Wa Kata Ya Bukoli,Wilayani Geita,Imemalizika  Huku Timu Ambayo Haijawai Kuwa Na Historia Ya Kuchezea Kichapo Ya Bugogo Fc  Imejikuta  Ikila Kichapo Cha Mabao  Mawili Na Timu Ya Nchimbi Boys Na Yenyewe Kuambulia Bao Moja Kwenye Dk 40 Kipindi Cha Kwanza.


Michuano Hiyo Ya Ligi Ya Faraji Cup Ilianza Kwa Mashindano Ya Sarakasi Huku Timu Za Wakongwe  Mavetirani Wakikumbushia Mchezo Wa Mpira Wa Miguu ,Na Saa Kumi Na Dk Hamsini Ndipo Mchezo Ulipoanza Kulindima Katika Viwanja Vya Ccm,Bukoli.

Mchezo Ulianza Kwa Bashishi Kubwa Sana Kutoka Kwa Timu Ya Bugogo Ambayo Ilionesha Kushambulia Mchezo Huo Kwa Nguvu Zaidi Katika Kipindi Cha Kwanza , Dk 40 
Marius Joseph  Aliweza Kuipatia Gori La Kwanza Timu Ya Bugogo.

Hadi Wanakwenda Mapumziko Timu Ya Bugogo Fc Ilionesha Kuwa Juu ,Baada Ya Mapumziko Mchezo Wa Pili Ulianza Kwa Kishindo Kikubwa Ambacho Kilianzishwa Na Timu Ya Nchimbi Fc Na Ndani Ya Dk 23 Kipindi  Cha Pili Peter Dotto,Aliweza Kuipatia Timu Ya Nchimbi Bao Moja Na Kuwa Sare Ya Bao Moja Kwa Timu Zote Mbili,Mchezo Uliendelea Na Ndani Ya Dk 36 Katika Kipindi Cha Pili Timu Hiyo Hiyo Ilipata Bao La Pili Lililofungwa Na Juma Dede Hadi Dk Tisini Zinamalizika Timu Ya Nchimbi Fc Ilikuwa Ikiongoza Kwa Mabao Mawili Kwa Moja Kutoka Kwa Bugogo.

Hata Hivyo Mchezo Huo Uligubikwa Na Fujo Katika Kipindi Cha Pili Ni Baada Ya Mchezaji Wa Timu Ya Bugogo ,Ibrahimu Kadele Kumpiga Ngumi Ndani Ya Uwanja Robart Steve Hali Ambayo Ilisababisha Mwamuzi Wa Timu Hizo Mbili  Kuwapa Kadi Nyekundu,Mwingine Aliyepatiwa Kadi Nyekundu Ni Ramadhani Abdu Wa Timu Ya Nchimbi Fc.

Hata Hivyo Mwandaaji Wa Michezo Hiyo,Ambae Ni Diwani Wa Kata Ya Bukoli,Faraji  Rajab ,Amewataka Wanamichezo Hao Kuungana Hili Kuendeleza Soka La Kata Hiyo.
“Natagemea Kwamba Ndani Ya Miaka Mitano Ya Uwongozi Wangu Niwapate Vijana 

Ambao Watafikia Hatua Ya Kucheza Supa Ligi Ya Vodacom”Alisema Faraji.
Kocha Wa Timu Ya Nchimbi Boys Fc,Zakaria Hamad,Alisema Kuwa Siri Kubwa Iliyowafanikisha Kuweza Kupata Ushindi Huo Ni Mazoezi Ambayo Wamekuwa Wakifanya Mala Kwa Mala.

Katika Michuano Hiyo Mshindi Wa Kwanza Amepatiwa Kitita Cha Sh,Laki Tatu,Na Kombe Wa Pili Akipatiwa Kiasi Cha Sh Laki Mbili Na Wa Tatu Laki Moja.



Share it:

Post A Comment: