Wanafunzi wa chuo cha Rice lise wagoma kuingia madarasani.

Share it:


Ni kibao kilichopo katika chuo cha Rich Rice kikikukaribisha chuoni hapo.


Wanachuo wakiwa katika hali ya mgomo wa kuto kuingia madarasani .


Wanachuo wakielekea kwenye Hostel .

Makamo mkuu wa chuo hicho Elisha Ndelembi akitoa maelezo kwa wanahabari juu ya hatua ya kugoma wanafunzi.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akitoa maelekezo mbele ya wanafunzi.
Wanachuo wakifatilia kwa makini maagizo ya Mkuu wa Wilaya.


Na Joel Maduka
Wanafunzi wa chuo cha uwalimu cha RICH LISE kilichopo mkoani Geita,wamegoma kuingia madarasani kwa kile kinachodaiwa ni kufutwa kwa kozi ya uwalimu wa cheke chekea ,hali ambayo imewasababisha kushindwa kujua mwafaka wao kwani ni muda sasa tangu waanze masomo chuoni hapo na taarifa hiyo imekuja muda ambao walikuwa hawadhani kutokea kwa jambo kama hilo na kusababisha kuwa na mshituko

Happynes Charles,ni mwanafunzi wa  chuo hicho,alisema kuwa  kero hizo zimewachosha kwani walimu wamekuwa wakiwazungusha na kushindwa kujua mwafaka wao ni nini”kiini cha kugoma jana mkurugenzi alitutangazia kwamba kozi tunayoisoma sisi haipo na kwamba wanafunzi wote hatujasajiliwa kwa hiyo ndio maana leo tumetaka kujua mwaka wetu kama tumesajiliwa au la  lakini tunashukuru tumejua ukweli wetu kwamba hatuna chetu hapa”alisema Happynes.

Hata hivyo sifa ya  wanafunzi wa uwalimu ni kuanzia kuwa na ngazi ya divitioni three,na wengi ambao wanalalamika kutokujua haki yao ya msingi ni wale ambao wana division four,Betrice Zakayo yeye ni mwanafunzi wa chuo hicho ambapo alisema kuwa yeye ni bora wapatiwe fedha zao waondoke huku akiomba serikali kuingilia kati swala hilo.”Mimi nina three lakini sitaki kusoma hapa masomo yanaanza mwezi wa kumi lakini sisi tuliambiwa tulipoti mwezi wa nane na hera zimeliwa zote na alikula hera ameondoka  turudishiwe pesa zetu zirudi kama mambo 
hayaeleweki twende vyuo vingine”alisema Beatrice.

Makamo wa chuo hicho,Bw,Elisha Ndelembi,alisema waliondoka kwenda nectar mwanza kwa lengo la kujua program hiyo”jambo hili ambalo limekuwa likienea sana  Kwamba ECD yani program hii wanayoendelea nay o wanachuo haijasajiliwa na muda wake umepita ilikuwa ni uko nyuma  mwisho wake ni 2015 basi tumekwenda tukakuta uwongozi wa necta kanda uko vizuri ukawa wazi sana wakasema kwamba tunasikitika mno na mmefanya vizuri kuja kwani hiyo ECD imeshafutwa na tulikuwa na mpango wa kuja kukifungia chuo hicho”alisema Ndelembi.

Mkuu wa wiaya ya Geita,Herman Kapufi amewataka wanafunzi hao kuwa watulivu huku akiagiza wakuu wa necta kufika chuoni hapo, afisa  taaluma na afisa elimu  kufika saa tatu ili kutatua changamoto zilizopo chuoni hapo.huku akiagiza idara ya uhasibu kuwa na kumbukumbu zote za malipo ya wanafunzi hao.




Share it:

Post A Comment: