AFUNGWA JERA MIAKA MITATU KWA UENDESHAJI HATARI

Share it:












MAHAKAMA ya Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita imemuhukumu Juma Pakara @Abdalah Wangu(44) kwenda kutumikia kifungo jera miaka mitatu kisha kufutiwa leseni ya Udereva kwa kosa la kusababisha kifo kutokana na uendeshaji Hatari.

Mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi Gabriel Kulwijira  mwendesha mashtaka wa Polisi Insp Neema Nhaluke mshtakiwa wa kesi Na 27/2016  juma  Mkazi wa mtaa na Kata ya Katente mjini Ushirombo Wilayani hapa.

Aliyekuwa anashtakiwa kwa kosa lakusababisha kifo kutokana na Uendeshaji Hatari kinyume na kif 40(1) 27(1)(a) cha 63(2) (a) cha sheria ya Usalama Barabarani sura Na 168 iliyofanyiwa marejeo 2002.

Insp Nhaluke alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo septemba 05 /2016 majra ya saa 2 za usiku katika Barabara ya Masumbwe Ushirombo kijiji cha Nasihukuru .

Alisema wakati juma akiendesha Gari lenye namba za usajiri T.920 DCA Toyota Town hiace min bus kwa mwendo kasi bila uangalifu alimgonga mtu ambaye hakujulikana jina lake wala mahali anakoishi wala aendako na kumsababishia Kifo.

Baada ya mshtakiwa kukiri kosa ndipo hakimu huyo makazi mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Bukombe Gabriel Kurwijila akamuhukumu Juma Pakana kwenda kutumikia kifungo jera miaka mitatu na kumfutia Leseni yake ya Udereva  ambapo hata pata kibari cha kuwa na Leseni kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mh, Kurwijila alisema hukumu hiyo ni kwa muujibu wa sheria isemayo Uendeshaji hatari na kusababisha kifo adhabu yake ni Kifungo, hivyo ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa madereva wengine wale wenye tabia ya kuvunja sheria ya Usalama Barabarani.

Na  Makunga Peter.
Share it:

habari

Post A Comment: