BRELA YAENDESHA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA MKOANI GEITA.

Share it:
Wafanyabiashara Mkoani Geita wakiwa katika semina.
Emil Kasagara akifanya  utambulisho.

Meza Kuu kushoto aliyevaa shati la maua ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga na katikati ni Mtendaji Mkuu Wa (BRELA) Frank Kanyusi

Mtendaji Mkuu Wa BRELA Frank Kanyusi Akitoa neno la kumkaribisha mgeni rasmi.

Wajumbe wa semina wakifatilia kwa makini semina hiyo.

Mgeni Rasimi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga  Akitoa Hotuba yake katika ufunguzi wa semina hiyo.


Afisa Mtendaji Wa TCCIA  Mkoani Geita  Mariam Mkaka,akitoa ufafanuzi juu ya namna ambavyo TCCIA imekuwa ikifanya kazi Mkoani hapo.
Picha ya pamoja  wafanyabiashara na mgeni rasmi Mkoani Geita.

Picha ya pamoja Mgeni Rasmi na wafanyakazi wa BRELA.
Kufuatia   Ugumu Na Changamoto Ambazo Wafanyabiashara Walikuwa Wakikutana Nazo Kusafiri Kwa Umbali Mrefu Kwenda Dar es  Salaam  Kwaajili  Ya Kufuata  Usajili Wa Biashara Na Kampuni Wameshukuru Kwa Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Leseni (BRELA)Kwa Kuweza Kuleta Huduma Ya Usajili Kwa Wiki Nzima Mkoani Geita.

Kauli Hiyo Wameisema Mapema Leo  Katika Semina Ambayo Imefanyikia Katika Ukumbi Wa Mikutano Ofisi Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Geita.

Lengo La Semina Hiyo  Ni Kuwajengea Uwezo Namna Ambavyo Wafanyabiashara Wadogo Na Wakubwa Wanaweza Kutumia Fursa Ya Kuinua Vipato Vyao Kwa Kusajili Biashara Na Kampuni Ambazo Wamekuwa Wakifanyia Shughuli Za Kila Siku.

Raphael Siyantemi Ni Mfanyabiashara Mkoani Geita,Amesema Kuwa Anaamini Kupitia Semina Hiyo Ambayo Imeandaliwa Na Brela Itamsaidia Zaidi Namna Ambavyo Anaweza Kusajili Kampuni Yake.

Nae Bi,Merry Mpangalala Ameongezea Kuwa Ni Vyema Kwa Brela Wakaona Namna Ambavyo Wanaweza Kuanzisha Vituo Katika Mikoa Ya Kanda Ya Ziwa Ambayo Itasaidia Kutoa Huduma Ya Usajili Kwa Urahisi Zaidi.

Aidha Kwa Upande Wake Afisa Mtendaji Wa TCCIA  Mkoani Geita  Mariam Mkaka,Ametaja Changamoto Wanazokutana Nazo Ni Pamoja Na Kurathimisha Majina Kwa Urahisi Kwa Wafanyabiashara Hivyo Wanaamini ujio wa  Brela Mkoani Hapa utatatua Changomoto Ambazo Zimekuwa Zikiwasumbua Kwa Muda Mrefu.

Kwa Upande Wake Mtendaji Mkuu Wa Brela Frank Kanyusi, Amesema Kuwa Wamejipanga Kutoa  Huduma Zote Za Usajili  Kwa Njia Ya Mtandao.

Hata Hivyo Kwa Upande Wake Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi Wa Semina Hiyo ,Mkuu Wa Mkoa Wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,Amewashukuru Brela Kwa Kutumia Njia Ya Kuleta Shughuli Ya Usajili Wa Biashara Kwani Anaamini Itasaidia Wafanyabiashara Kupunguza Gharama Za Kwenda Dar Es Salaam Kwaajili Ya Usajili.

Imeandaliwa na Joel Maduka


Share it:

habari

Post A Comment: