GEITA,BABA AJIUA BAADA YA KUMUUA BINTI YAKE.

Share it:
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli
Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Geita Mponjoli Mwabulambo akithibitisha kutokea kwa tukio hilo ofisini kwake.


GEITA:Mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Martha Charles Mwenye umri wa miaka 15 ameuwawa kwa kupigwa  na fimbo na Baba yake mzazi kisha baba yake aliyefahamika kwa jina la Charles Mlima  kujinyonga baada ya tukio hilo lilitokea  katika kata na kijiji cha kaseme wilayani na Mkoani  Geita.

Maduka oline imefika kijijini hapo na kujionea watu wakiwa katika majonzi na huzuni kubwa baada ya misiba hiyo miwili.

Akizungumza  na Madukaonline ndugu wa familia hiyo John Lufunguro  amesema  kuwa marehemu ambae ni mtoto wa Baba huyo alikumbwa na mauti hayo  baada ya kupigwa na baba yake kwa kile kilichodaiwa kuwa  amekutwa katika hali ya kimapenzi, hali ambayo haikumpendeza baba yake kutokana na kuwa na umri mdogo kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.

“Hee tukio hili yeye mwenyewe baba mji alimkuta mwanawe akiwa katika hali ya kimapenzi na baada ya kuona hivyo alimkimbiza binti yake na kuanza kumpiga na baada ya kumpiga mtoto alizidiwa na mwisho wa siku yeye alikimbia maporini na kujinyonga kwa kuhofiwa kukamatwa marehemu ameacha mke na watoto watano.”alisema Lufunguro.

Mke wa  Marehemu Mariam Chares  ameiambia Madukaoline  kuwa mume wake alimkuta katika biashara yake ya kila siku na kumwambia anatakiwa kwenda nyumbani haraka kwani Binti yao ana hali mbaya sana, na baada ya kufika nyumbani alimkuta binti akilia na kulalamika kuwa baba yake amemuua.

“Nilimkuta Binti yangu akiwa anagalagala huku damu zikimtoka nyingi na akisema kuwa baba amenihua mama”alisema Mariam

Naye Diwani wa kata hiyo Andrew  Karamula amelaani tukio  hilo na amewataka wananchi kuachana na tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kutokomeza matukio ya namna hiyo.

Aidha Kamanda wa polisi mkoani Geita Mponjoli  Mwabulambo   amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akitaja chanzo cha tukio ni Baba kumkuta mtoto wake akiwa na mwanaume.



Share it:

matukio

Post A Comment: