GGM WATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA SUMU GEITA.

Share it:
Meneja mahusiano ya jamii wa  GGM,Manase Ndoloma akiteta na wananchi ambao wameathirika na sumu ya sayanaidi  wakiwa kwenye zahanati ya Busanda.
Wananchi wakiendelea kusubilia kupatiwa  huduma ya kwanza kutokana na kulamba na kunusa sumu hiyo.

Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Busanda,Steven Masesa akifafanua jambo na namna ambavyo wao kama zahanti wamefanikisha kutoa huduma.

Mgonjwa akiwa amezidiwa akiwa nje amelala.



Mtaalam wa maswala ya uokoaji kutoka kampuni ya GGM ,Paul Kagondi akitoa elimu namna ambavyo wananchi wanaweza wakajikinga ili wasiathirike na sumu ya sayonaidi.

Mtaalam akionesha kifaa cha kukagulia sumu  hiyo.

Mtaalam akikagua na kuonesha  sumu hiyo ambayo imeonekana maeneo ya kijiji cha Busanda ikiwa imetapakaa. 

Wataalam wakiendelea na ukaguzi katika maeneo ya kijiji cha Busanda.



 GEITA:Kampuni ya uchimbaji wa madini Mkoani Geita (GGM) Imepeleka wataalam na madaktari katika kijiji na kata ya Busanda Wilayani Geita lengo likiwa ni kutoa huduma kwa waathirika wa sumu ya sayanadi.


Siku ya jumapili September 11 ,Mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Simomo Waziri( 4) alifariki dunia na huku mifugo 30 ikipoteza maisha baada ya kulamba kitu kinachosadikika kuwa ni  sumu ya sayonidi iliokuwa ikisafilishwa kwa usafiri  bodaboda bira kuhifadhiwa vizuri.

Akizungumza  na waandishi wa Habari Meneja  Mausiano ya jamii  wa mgodi wa GGM  Manase Ndoloma Alisema wameamua kupeleka wataalam  na madokta ili kuwasaidia waathirika nah ii ni kutokana ma mahusiano mazuri waliyonayo na wananchi wanaouzunguka mgodi.

“Sisi kama mgodi ambao tupo Mkoani hapa tuliguswa na tukio hili baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari na kwasababu ni swala ambalo lipo ndani ya uwezo wetu ndio maana tumeamua kutuma wataala na kusaidia tatizo hili.”alisema Ndoloma.

Baadhi ya waathirika  wengi wao wakiwa ni watoto wadogo   walikuwa wamekusanyika katika  zahanati ya Busanda walieleza madhara walioyapata baada ya kunusa na kulamba sumu hiyo kuwa wamekuwa wakijisikia tumbo kuuma na kizunguzungu kikali .
.
 Mtaalam wa maswala ya sumu ya Sayanaidi kutoka ndani ya Mgodi huo Paul Kagondi amekili  kuwepo kwa sumu hiyo ya Sayanaidi katika eneo hilo na kwamba wameshafanya uchunguzi na kuakikisha wanatatua tatizo ambalo limetokea kijijini hapo.

 “Tumefika kijijini hapa na tumefanya uchunguzi na kubaini kweli kulikuwa na sumu hiyo lakini tumeshafanya uchunguzi na kutatua tatizo la sumu hiyo ambayo ilikuwa imesambaa”alisema Kagondi.

Imeandaliwa na Joel Maduka.





Share it:

matukio

Post A Comment: