KILIMANJARO QUEENS YAJIWEKA SAWA CECAFA .

Share it:






Kikosi kikiwa katika utulivu.

Kikosi cha Kilimanjaro Queen kikiwa katika mazoezi.
Timu ya Tanzania bara ya Wanawake Kilimanjaro Queen,imeanza maandaliza ya CECAFA kwa kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Timu ya Wanawake wa Burundi mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana.

Akizungumza kwa njia ya simu ,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Sebastian Nkoma,amesema kuwa kweli nimeweza kupata ushindi wa magoli matatu katika mchezo wangu wa kwanza nikiwa na timu hiyo japo kuwa mchezo haukuwa rahisi ila vijana wangu wananipa matumaini ya kufanya vizuri michuano ya wanawake yanayotarajia kuanza Septemba 11,mwaka huu nchini Uganda.

“Unajua kama timu mnaanza kwa ushindi tena timu kubwa kama Burundi ambayo nayo inashiriki michuano hiyo ni dalili njema kuwa tutakuja na ubingwa kwani tunaenda kupigana mwanzo mwisho ila tunajua tupo kundi ngumu ambalo linajumuisha Ethiopia na Rwanda hivyo tunawaomba watanzania watuombee tufanye vizuri”alisema Nkoma

Kilimanjaro Queens ilipata magoli yake dhidi ya Burundi kwa kupitia wachezaji wake mahiri Asha Rashid,Mwanahamis Omary “Gaucho’ na moja wakijifunga kutokana na piga ni kupige katika lango lao na Timu hizo mbili zinatarajia kuondoka Leo Bukoba na kuelekea nchini Uganda kwa michuano hiyo inayotarajia kuanza siku ya Jumapili.

Michuano hii kwa upande wa Wanawake ni kwa mara ya kwanza inaanzishwa katika ukanda huu wa CECAFA hivyo ni fursa kwa timu za wanawake kufanya vizuri na kujimarisha katika mashindano ya CAF na zimegawanywa katika makundi mawili.
Kundi A:                                                                                           Kundi B:
.Kenya                                                                                              Kilimanjaro Queens.
.Uganda                                                                                             Rwanda.
.Burundi                                                                                            Ethiopia
.Zanzibar

Kilimanjaro Queens inatarajia kutupa karata yake ya kwanza Septemba 12 kucheza na Rwanda kabla ya kumalizana na Ethiopia Septemba 16 na Zanzibar wao wataanza na Burundi Septemba 11 na wenyeji nao watacheza na Kenya siku hiyo hiyo.
Share it:

michezo

Post A Comment: