RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE

Share it:
Hudson Kamoga akiwa kwenye majukumu ya kila siku.

Horodha ya uteuzi.




Rais  John Magufuli leoamemteua Eliya Ntandu kuwa Katibu  Tawala wa Mkoa wa Songwe.


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.
Imeeleza kuwa Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana ambao ni Ado Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na Tixon Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Wakati huo huo, Rais  Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mmoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa moja ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo Godwin  Kunambi(Manispaa ya Dodoma), Elias Ntiruhungwa(Mji wa Tarime),  Mwantumu Dau( Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba), Frank Bahati(Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe), Hudson Kamoga(Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu), Mwailwa Pangani(Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo).
Wengine ni  Godfrey Sanga(Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama), Yusuf Semuguruka(Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga), Bakari Mohamed(Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea),  Juma  Mnwele(Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo), Butamo Ndalahwa(Halmashauri ya Wilaya ya Moshi),  Waziri Mourice( Halmashauri ya Wilaya ya Karatu) na  Fatma  Latu( Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo)






Share it:

habari

michezo

Post A Comment: