Wanafunzi wilayani Geita wametakiwa Kusoma kwa Bidii.

Share it:
Mkuu wa  Wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rwamgasa.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Rwamgasa wakifatilia kwa makini kile ambacho alikuwa akikizungumza mkuu wa wilaya.


Na Joel Maduka
Mkuu wa wilaya ya Geita ,Hermani Kapufi amewataka wanafunzi wilayani hapo kusoma kwa bidii na kuongeza nguvu zaidi katika masomo yao ni kutokana na kwamba kwa sasa nchi hipo katika utandawazi hivyo wasomi wanaitajika sana katika taifa ili kuondokana na changamoto ambazo zinalikabili Taifa.

wito huo ameutoa wakati alipokuwa katika ziara yake ya kikazi katika kata ya Rwamgasa,Kapufi alisema kuwa ni vyema kwa wanafunzi kuona sababu ya kutumia muda wao walionao pindi wanapokuwa shuleni kwa bidii zaidi na kuachana na tabia ya kujiingiza katika makundi ambayo yanaharibu mustakabali wa maisha yao.

"Tunatambua kuwa serikali imeweka fedha nyingi na pia wazazi wanatumia nguvu nyingi kuakikisha mnasoma hivyo ni vyema na nyinyi mkawiwa kusoma kwa bidii na kuachana na tamaa ambazo zitawaharibia masomo yao"alisema Kapufi.

Aidha amempongeza diwani wa Kata hiyo kwa juhudi zake za kuakikisha kwamba wanajenga mahabara ya kisasa katika shule hiyo.

Share it:

matukio

Post A Comment: