Mfano wa Hundi ya Milioni 30,ikikabidhiwa kwa mgeni rasmi pamoja na Mkurugenzi wa Nelico na Mratibu wa Briggitte Alfred,ambazo zimetolewa na mgodi wa dhahabu wa GGM.
Suala la Unyanyapaa pamoja na ugongwa wa saratani ya
ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) ni tatizo ambalo
limeendelea kuwafanya kuishi kwa mashaka
katika familia na jamii zinazowazunguka.
kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa shirika la kusaidia
watoto na watu wenye ulemavu (NELIKO) Paulina Alex wakati wa uzinduzi wa mradi kuwajengea
uwezo, na kutoa elimu kuhusu afya na namna ya kujilinda kwa watu wenye ulemavu
wa ngozi albino.
uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Yahana Memorial Centre uliopo mjini Geita.
Paulina amesema Ugongwa wa saratani ya ngozi kwa wenye ulemavu wa ngozi (albino) ni kikwazo
kikubwa sana na kwamba kwa wilaya ya Geita kuna wagonjwa watano (5) wanaohitaji
msaada wa matibabu kutokana na hali zao kuwa mbaya.
“katika wilaya
yako ya Geita kuna watu wenye albinism watano ambao ni wagonjwa wa kansa
wanahitaji msaada mkubwa sana na kuna watu wenye albinism wawili ambao wao
imefikia kasa yao kwenye hatua ya nne ni sikitiko kidogo swala hili tujaribu
kulipa
kipaumbele ili kuwasaidia wenzetu changamoto nyingine
ni swala la unyanyapaa katika familia zetu bado ni tatizo”alisema Paulina
Mwenyekiti wa Tas
wilaya ya Geita, Lazaro Malendeja amesema
kuwa maradhi ya saratani yamekuwa ni adui mkubwa sana ambae anasumbua watu
wenye ualbino na hii ni kutokana na changamoto kubwa ya kukosekana kwa huduma
ya afya katika upande wa saratani kwani mara nyingi wamekuwa wakienda jijini Dar
es salaam kutibiwa hivyo ameomba kwa serikali kuona umuhimu wa kuleta kitengo
cha huduma ya saratani katika hosptali zilizopo mkoani hapa.
Naye makamu wa rais
wa mgodi wa dhahabu wa Geita
(GGM) Simoni Shayo amewataka
wachimbaji kuacha imani potofu ya kwamba
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yanasababisha upate utajiri huku walengwa wa
mradi huo wakipongeza kwa kupewa msaada
huo.
Akizungumza wakati wa kufunga uzinduzi huo kwa niaba
ya mkuu wa mkoa wa Geita,mkuu wa wilaya ya Geita mh Herman Kapufi amesema serikali mkoani hapa imejipanga kuwakamata na kuwachukulia hatua
kali watu ambao wamekuwa wakitishia
maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
kampuni ya kuchimba madini ya dhahabu ya Geita (GGM)
mkoa wa Geita katika kuunga mkono juhudi za kupinga mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi imetoa hundi ya
kiasi cha sh milioni thelathini (30) kwa ajili ya kuwezesha jambo hilo, huku
wakiomba fedha ziwafikie walengwa.
|
Post A Comment: