|
Afisa mahusiano wa GGM Manase Ndoloma akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana nyakumbu umuhimu wa kupenda kusoma vitabu ni kwenye uzinduzi wa maktaba katika shule hiyo ulio fanyika leo tarehe 17 Oktoba. |
|
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Nyakumbu wakifatilia kwa umakini yale ambayo alikuwa akiyazungumza afisa mahusiano. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita ambae alikuwa ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Herman Kapufi akisalimiana na baadhi ya wanafunzi na walimu baada ya kuwasili katika viwanja vya shule hiyo. |
|
Wanafunzi wakiimba nyimbo ya shule ya wasichana ya Nyakumbu. |
|
Walimu wa shule hiyo pia wakiimba nyimbo ya shule hiyo. |
|
Mwanafunzi akionesha umahiri wake wa kupiga Ngoma mbele ya mgeni rasmi katika shughuli ya uzinduzi wa maktaba. |
|
Kikundi cha ngoma shuleni hapo kikionesha burudani ya ngoma kutoka mkoani Kagera. |
|
Kashindi Emmanuel kutoka shirika lisilo la kiserikali la Read International akisoma risala mbele ya mgeni huku akielezea namna ambavyo walivyofanikiwa kuweza kufanikisha Maktaba hiyo kwa kushirikiana na Mgodi wa GGM. |
|
Msemaji wa shirika lisilo la Kiserikali la Read International Stella Mtega,akishukuru kwa GGM kwa kufanikisha kutoa fedha ambazo zimesaidia kununua vitabu kwaajili ya maktaba. |
|
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akisoma kitabu kiitwacho"DUNIA YA FEDHA"ambacho amekiandika yeye na pia amekigawa shuleni hapo kwaajili ya wanafunzi kukisoma. |
|
Mwalimu Mkuu wa shule ya wasichana ya Nyakumbu Georgia Mgashe akipokea kitabu kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Geita. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizindua maktaba ya kisasa iliyopo shule ya wasichana ya nyakumbu iliyopo kata ya Nyakumbu. |
|
Mkuu wa wilaya akikagua baadhi ya vitabu vilivyopo katika maktaba hiyo. |
GEITA :Jumla ya kiasi cha sh milioni ishirini (20) kimetolewa na mgodi wa
dhahabu wa Geita (GGM) kwenye shule ya Sekondari ya wasichana ya Nyankumbu
iliyopo wilayani na mkoani Geita lengo ikiwa ni kuweka vitabu vya kutosha
katika maktaba ya shule hiyo.
Akizungumzia changamoto
ambazo walikuwa wakikutana nazo wanafunzi wa shule hiyo,Hajira Salum na
Verediana Traphone wamesema kuwa changamoto ya uhaba wa vitabu shuleni hapo
ilikuwa ni moja wapo ya kikwazo
kilichokuwa kikisababisha wanafunzi kutokufanya vizuri shuleni hapo .
Aidha kwa upande wake Afisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa GGM
Manase Ndoroma,amewasisitiza wanafunzi hao kujenga desturi ya kusoma kwa bidii
vitabu ili kuendana na Dunia ya sayansi na teknolojia.
“Tunatambua kuna faida
nyingi sana katika kusoma vitabu, hivyo ni muhimu nyie wanafun zi kutumia
maktaba hii kwa kusoma vitabu vingi zaidi kwani kuna mambo mengi mazuri katika
kujisomea na tuombe mashirika mengine ni
vyema yakajitokeza kuchangia maendeleo ya elimu nchini”Alisema Manase.
Mwalimu mkuu wa shule
hiyo,Georgia Mgashe,amefafanua kuwa vitabu hivyo vitakuwa msaada
mkubwa kwa shule hiyo kwani hakutakuwa na kisingizio cha kukosekana kwa vitabu
shuleni hapo .
“Imani yangu ni kwamba kwa
sasa wanafunzi watasoma kwa bidii na kujituma zaidi kwani hakuna kisingizio cha
kukosekana kwa vitabu tumeona GGM wameweka vitabu vingi katika maktaba
yetu”Alisema Mgashe.
Msemaji wa Read
internation Stella Mtega ,ametoa shukrani kwa mgodi wa dhahabu
wa GGM kwa kuwezesha ufadhili vitabu
vingi katika maktaba hiyo.
Akizindua Maktaba hiyo Mgeni
rasmi ambae ni mkuu wa wilaya ya Geita mh Herma Kapufi amewasisitiza wanafunzi
kutunza vifaa na vitabu vilivyonunuliwa
ili viweze kuja kutumiwa na wanafunzi wengine.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: