Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu
mbalimbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji
viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
|
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya
mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
|
Baadhi
ya wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji
viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. |
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (katikati) akifuatilia
mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau mbalimbali wakati uzinduzi wa matokeo
ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar
es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
|
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kulia) akiteta jambo
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru wakati wa uzinduzi wa matokeo
ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar
es Salaam.
|
(PICHA
NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
DAR ES SALAAM :SERIKALI imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana
na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani
(UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili
kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam NA
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt,Charles Mwijage wakati wa uzinduzi
wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.
Dkt Mwijage
alisema kuwa katika mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini,
Malaysia na Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango cha juu
zaidi kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.
Alisema
katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya viwanda vidogo vinavyopatikana nchini, Wizara yake
imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo
vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia
nchi kukua kiuchumi .
“Asilimia
25- 40 ya mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani,
katika kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo
vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao
yao” alisema Mwijage.
Aidha, Dkt
Mwijage alisema, sekta ya viwanda vidogo vidogo nchini imeendelea kukua kwa
kasi nchini ambapo hadi sasa kuna jumla ya viwanda 3800 vilivyoanzishwa nchini
kuanzia Novemba 2015 hadi octoba, 2016.
Katika hatua
hiyo Dkt Mwijage alisema kuwa Wizara yake inaendelea kuhamasisha Sekta binafsi
kuwekeza katika Sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ikiwa jukumu kuu
la Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na inajenga mazingira wezeshi
kwenye sekta binafsi kuzalisha na kufanya biashara.
Naye
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alisema kuwa
matokeo hayo yanaonyesha mafanikio katika sekta ya viwanda ikiwemo kuongezeka
kwa ajira zipatazo 264,223 nchini na kuchangia uchumi kwa takribani Shilingi
bilioni 8.0 kwa mwaka 2013.
Alisema kuwa
Takwimu za matokeo ya sense ya uzalishaji viwandani ni rasmi na kuwataka
watunga sera, wanasiasa, viongozi, sekta binafsi na watu binafsi kutumia matokeo hayo kwa lengo la kuboresha Sekta ya
viwanda nchini.
Imeandaliwa na Beatrice Lyimo(Maelezo)
Post A Comment: