Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi akizindua kampeni ya Longa na Takururu kwenye zoezi lililofanyika katika viwanja vya Kalangalala Wilayani Geita. |
Mkuu wa wilaya Herman Kapufi akisalimiana na wananchi ambao walifika katika uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo itasaidia kutoa taarifa kwa wepesi zaidi. |
Mkuu wa wilaya akipokea taarifa ya takukuru kutoka kwa mkuu wa takukuru Mkoani Hapa,Bw Thomas Ndalo baada ya kusoma na kuelezea kusudi la kuwepo kwa kampeni. |
Wanafunzi wa shule ya sekondali ya Geita wakifatilia kwa makini burudani mbali mbali zilizokuwa zikiendelea katika viwanja vya kalangalala. |
Kwaya ya Mgusu ikiimba na kuburudisha katika uzinduzi wa kampeni hiyo. |
Mgeni Rasmi akihesabu pesa kwaajili ya kuwatunza waimbaji kutoka kikundi cha Mgusu. |
Mkuu wa Takukuru mkoani Geita,Thobias Ndalo akielezea namna ambavyo zoezi la kupiga 113 litakavyoleta manufaa kwa wananchi na kutokomeza vitendo viovu vya rushwa. |
Mchungaji wa kanisa la seventh day Adventist Paul Kwilasa,akisoma neno la Mungu kutoka katika kitabu cha zaburi ambacho kimeelezea namna ambavyo rushwa inaweza kuondoa amani ya nchi. |
GEITA:Taasisi
ya kuzuia na kupamba na Rushwa Wilayani na Mkoani Geita,imezindua kampeni ya
Longa nasi lengo ikiwa ni kutoa taarifa kwa wepesi kwa wananchi dhidi ya
vitendo vya rushwa ambavyo vimekuwa vikijitokeza mala kwa mala.
Akizungumza
katika viwanja vya kalangalala ambapo zoezi la uzinduzi limefanyikia hapo ,Mkuu
wa Takukuru mkoani humo,Thobias Ndalo, ameelezea kuwa rushwa ina madhara makubwa
kwa Taifa ambapo
imekuwa ikipokonya haki kwa wananchi,na imekuwa ikikosesha
serikali mapato hali ambayo imesababisha
serikali kushindwa kutoa huduma bora kwa
wakati.amesisitiza kwa kuendelea kueleza kuwa Rushwa inaua,inatia ulemavu
wananchi na kuongeza umasikini sababu hizo ni moja wapo ya kuhifanya taasisi
hiyo pamoja na wananchi kupambana na rushwa kwa nguvu na maarifa ya hali ya
juu.
“Pamoja na
kuwa rushwa ni kosa la jinai ,lakini katika imani za dini zetu rushwa ni dhambi
.Niwaombe wananchi wote pamoja na viongozi wa dini mliopo hapa kutumia na
kuzingatia mafundisho ya dini zetu pia katika kukabili tatizo la rushwa katika
jamii,nadhani mtakubaliana name kuwa tukiacha rushwa ishamiri hata uhuru wa
kuabudu hautakuwepo kwa sababu moja ya madhara makubwa ya kukithiri kwa vitendo
vya rushwa ni vita.”Alisisitiza Ndalo.
Akinukuu
maneno ya Rais Magufuli aliyoyatamka
wakati wa uzinduzi wa Bunge novembe 20 mwaka jana kuhusu mapambano ya rushwa Mh Rais alisema"Jambo
moja nililolisema kwa nguvu kubwa wakati wa kampeni ni mapambano dhidi ya
rushwa na ufisadi ,sikufanya hivyo kwa sababu nilitaka tu kuwarubuni wananchi
ili wanipe kura zao na kunifanya kuwa Rais wao.Nililiongea jambo hili kwa dhati
kabisa ,na nilichokisema na kuwaahidi wananchi ndio hasa nilichokikusudia”.
Mkuu wa
wilaya ya Geita,Herman Kapufi ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika shughuli
hiyo,amesema kuwa serikali wilayani humo itaendelea kupinga vikali swala la
rushwa na kwamba kila mtu anawajibu wa
kukomesha vitendo vya rushwa na sio mzigo kuachia serikali .
Mchungaji wa
kanisa la seventh day Adventist Paul Kwilasa,amewashauri viongozi wa dini
kufundisha maadili mema kwa wahumini wao
ili kuepukana na vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kutokomezwa.
Imeandaliwa
na Madukaonline
Post A Comment: