Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi akikabidhiwa Mabati bando 20 na Mkurugenzi wa kampuni ya MUYA INVESTMENT Jua Kali Mkono kwenye ujenzi wa shule ya msingi Bwawani. |
Meneja wa kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya ANDLU GOLDEN AND PATINZI Kurwa Sagwea amekabidhi sh milioni 2 kwaajili ya mchango wa madawati katika shule ya msingi Subola kata ya Kaseme |
Mkuu wa wilaya ya Geita ,Herman Kapufi akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule hiyo. |
Mkuu wa wilaya akisalimiana na wananchi baada ya kuweka jiwe la Msingi. |
Mkuu wa wilaya akizungumza na wananchi wa kata ya Ludete huku akiwahimiza kupenda kuchangia maendeleo katika Kata hiyo. |
Picha ya pamoja na wafanyakazi wa MUYA INVESTMENT ambao ni wadhamini wakubwa katika ujenzi wa shule hiyo. |
Moja kati ya wananchi wa mta wa njia panda Bi,Amisa Salum akishukuru kwa jitihada ambazo zinafanywa na serikali za kuondoa changamoto ya elimu nchini. |
WANANCHI wa kitongoji cha njia panda kata ya
Ludete wilaya na mkoa wa Geita wamesema kuwa kujengwa kwa shule ya msingi
Bwawani kutasaidia kupunguza ajali za barabarani kwa wanafunzi
ambao walikuwa wakitembea umbali wa mrefu kufuata elimu.
Hayo wameyasema wakati wa kupokea msaada wa mabati bando 20 zenye thamani ya
sh.milioni 5.8 yaliyotolewa na
kampuni ya( WUZHOU INVESTMENT COMPANY LTD) ambao wanaojihusisha na uuzaji wa pikipiki aina ya
San LG pamoja na vipuri .
Wananchi
wamesema kuwa kujengwa kwa
shule hiyo kwenye kata yao pamoja na kampuni hiyo kuchangia mabati
kutasaidia watoto kuacha kutembea umbali mrefu hali iliyokuwa inasababisha vifo
wakati wa kuvuka barabara kwa watoto pindi waendapo shuleni.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi mtendaji wa kata
ya Ludete Aloyce Kamuli ameeleza kuwa pamoja na zoezi la kuendelea kujenga
shule ya msingi ya Bwawani lakini bado wanachangamoto kubwa zaidi ya kukosekana
shule ya sekondari katika kata hiyo hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi
waliopo katani hapo kutembea umbali wa kilomita nyingi kufata elimu.
Akikabidhi msaada huo msemaji wa kampuni ya muya
investment kanda ya ziwa Rashid Hasan
amefafanua kuwa lengo la kutoa mabati hayo ni kuunga jitihada za Raisi John Magufuli za kuinua elimu nchini na kupambana na
changamoto ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara katika shule zilizopo nchini
hapa.
Wakati huo huo meneja wa kampuni ya uchimbaji wa
dhahabu ya ANDLU GOLDEN AND PATINZI Kurwa Sagwea amekabidhi sh milioni 2
kwa ajili ya madawati katika shule ya msingi Subola kata ya kaseme huku mkuu wa shule hiyo Steven Kibiliti akielezea
kuwa bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madarasa shuleni hapo.
Akipokea misaada hiyo mkuu wa wilaya ya Geita
Hermani Kapufi amepongeza makapuni hayo na kusema kwamba kwa kutoa msaada wao
kwa moyo wanajiwekea hadhina mbinguni na kuwataka wengine kuiga mifano ya
kuchangia maendeleo yao kwenye maeneo wanayoishi.
Post A Comment: