GEITA:WASANII WA MAIGIZO WAMEITAKA JAMII KUWA NA MWITIKIO KATIKA UCHANGIAJI WA DAMU

Share it:
Baadhi ya wananchi na wasanii wa maigizo wakiwa katika zoezi la uchangiaji wa damu Mkoani Geita.

Wenyekiti wa chama cha wa sanii wa maigizo Mkoani Geita,Rosemery Michael akizungumza na waandishi wa habari juu ya shughuli ya uchangiaji wa damu.

Wananchi wa waliojitokeza wakifatilia burudani zilizokuwa zikiendelea katika viwanja vya kalangalala.

Meza kuu wakifatilia kwa makini zaidi burudani kutoka kwa mchekeshaji anayejulikana kwa jina la Mrugaruga wakati alipokuwa akitoa burudani ya vichekesho katika uwanja huo. 

Msanii wa sanaa ya vichekesho maarufu kwa jina la mruga ruga akijaribu kutoa vichekesho na kuigiza sauti ya viongozi mbali mbali wa hapa nchini na nje ya nchi.

 Chama cha waigizaji mkoani Geita,kimejitolea na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu lengo likiwa ni kunusuru maisha ya wale ambao wamekuwa wakiishiwa damu pindi wanapokuwa katika vituo vya afya,zahanati na hospitali hususani wakina mama wajawazito wanaokwenda kujifungua na wale ambao wamepatwa na ajali.

Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya kalangalala wilaya na mkoa wa Geita huku likiwahusisha wasanii mbali mbali kutoka katika wilaya zote zilizomo Mkoani humo.

Akizungumza na madukaonline,mwenyekiti wa chama hicho,Rosemary Michael,amefafanua kuwa wao kama kioo cha jamii wameguswa kwa kiasi kikubwa kutokana na tatizo la uhaba wa damu katika hospitali  hali ambayo imekuwa ikisababisha watanzania wengi kupoteza maisha kutokana na uhaba huo.

“Sisi kilichotugusa  ni  baada ya kuona  watanzania wengi  wanapoteza maisha kwa changamoto ya kukoswa damu na namna ambavyo tumeona Rais amekuwa akihamasisha  wananchi kujitokeza katika uchangiaji wa damu katika jamii hali hii imetugusa na kuona tunaweza kufanya jambo hili kwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu”Alisema Rosemery.

Kwa upande wake kiongozi wa damu salama Mkoani hapa,Alfredina Fredrick,ameelezea kuwa mwitikio wa watu sio mzuri kutokana na watu wengi kushindwa kujitokeza kuchangia damu  kutokana na kuofia afya zao lakini bado wameendelea kutoa elimu kwa wananchi  kuona umuhimu wa kujitolea damu.

Hata hivyo wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo wamesema kuwa ni vyema kwa serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kujitolea kuchangia damu kwani bado kunadhana potofu katika jamii zetu kuwa damu inapochangiwa baadhi ya hosptali huuzwa kwa wagonjwa jambo ambalo sio sahihi.



Share it:

michezo

Post A Comment: