BEKI wa kulia wa Klabu ya Azam FC, Shoamri Kapombe anatarajia kurejea dimbani Ijumaa hii katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar baada ya kusumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu,
Kapombe alikuwa nje kwa mechi sita baada ya kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja aliyoyapata katika mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Simba na kushindwa kumalizia mchezo huo huku timu yake ikipoteza mchezo huo kwa kufungwa 1-0.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo inaeleza kuwa, jopo la utabibu la klabu hiyo chini ya mtaalamu wa viungo Sergio Perez Soto na mganga mkuu wa timu hiyo, Mwanandi Mwankena leo asubuhi wamemruhusu Kapombe kuanza mazoezi na wenzake baada ya wiki iliyopita kumaliza programu ya mazoezi mepesi.
Hata hivyo, Soto alitoa kauli ya kuwa Kapombe yuko vizuri hivi sasa na malengo yao makubwa ni kuwemo kwenye orodha ya wachezaji wa Azam FC watakoivaa Kagera Sugar katika mchezo wa raundi ya 13 ya Ligi Kuu.
Kurejea kwa Kapombe katika kikosi cha Azam FC huwenda kukaongeza kitu cha ziada katika timu hiyo kutokana na uwezo wake alionao wa kupandisha mashambulizi pamoja na kufunga kama alivyofanya katika msimu uliomalizika.
Liacha ya kuwa na mwenendo mbaya kwa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu kutokuwa na matokeo yake kutokuwa mazuri, bado kikosi cha timu hiyo kina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo unaofuata dhidi ya Kagera Sugar kutokana na ushin di waliopata katika mchezo uliopita dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Azam Complex.
Post A Comment: