MBUNGE KANYASU AWASHUKIA WAKANDARASI JASCO UJENZI BARABARA YA GGM

Share it:
Wajumbe wa Bodi wakisikiliza kwa makini kile ambacho kilikuwa kikijadiliwa juu ya ujenzi wa barabara ya GGM yenye kilomita tatu ambayo inaunganika na mzunguko ambao upo katikakati ya mji wa Geita.

Mbunge wa Jimbo la Busanda Mkoani Geita,Mh Lorencian Bukwimba akielezea namna ambavyo wanaweza kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya barabara Mkoani Geita,ambae pia ni mkuu wa mkoa meja jenerali mstafu Ezekiel Kyunga akimtaka mkandarasi kuharakisha ujenzi wa Barabara Hiyo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita,Celestin Gesimba akifungua Mkutano huo na kumkaribisha mwenyekiti wa Mkutano.





Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Costatine Kanyasu akielezea namna ambavyo barabara inayotoka  GGM kuelekea kwenye mzunguko ilivyoharibu miundo mbinu ya eneo hilo



GEITA: Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kilomita tatu  Inayosimamiwa Na Mkandarasi Wa Jasco Inayotoka Mgodi Wa Dhahabu Wa GGM Kuja Katika Mzunguko Wa Magari Uliopo Mjini Umeonekana Kuwa Ni Changamoto Kubwa Kutokana Na  Kuchukua Muda Mrefu Bila Ya Kukamilika  Ujenzi Wake.


Akizungumza Katika Kikao Cha Bodi Ya Barabara Mkoani Hapa   Mbunge Wa Geita Mjini Constatine Kanyasu,Amesema Kuwa Kumekuwepo Na Kero Nyingi Kutoka Kwa Wananchi Kutokana Na  Kuharibiwa Kwa Miundo Mbinu Tangu Kuanza Kwa Ujenzi Wa Barabara Hiyo Na Kwamba Imechukua Muda Mrefu Hali Ambayo Imepelekea Kuwa Na Wasi Wasi Na Mkandarasi Ambae Anajenga Barabara  Na Kwamba Yawezekana  Uwezo Wake Kuwa Ni Mdogo.

“Tunamashaka na mkandarasi huyo kwani ni miezi mitatu sasa tangu ujenzi huanze lakini bado hatuoni jitihada zikifanyika katika kumaliza ujenzi huo mimi nafikilia sisi kama bodi tuje twende tukajione namna ambavyo ujenzi huo unasua sua.”alisema Kanyasu.

Kutokana Na Swala Hilo La Barabara Mwenyekiti Wa Bodi Hiyo Ambae Ni Mkuu Wa Mkoa Wa Geita,Meja Jenerali Mstafu Ezekiel Kyunga Amefafanua Kuwa Ni Wajibu Wa Mkandarasi Kumaliza Ujenzi Huo Katika Wakati Uliopangwa  Hili Kupunguza Changamoto Ambayo Wananchi Imekuwa Ikiwakabili Katika Eneo Hilo.

Akijibu Hoja Hiyo,Msimamizi Wa Barabara Hiyo Mwandisi  Kepucheki Mango,Ameeleza  Changamoto Ya Kutokukamilika Kwa Wakati Ujenzi Huo Ni Kutokana Na Kukutana Na Mwamba Kwa Baadhi Ya Maeneo Wakati Wa Ujenzi Huo .

“Ujenzi wa barabara umechelewa kutokana na kukutana na mwamba mgumu wakati wa ujenzi wa barabara hiyo na kwamba kwahiyo uchimbaji umechukua muda mrefu lakini kwasasa mkandarasi ameongeza vifaa vya kazi na anatarajia kuanzia December hataanza kuweka rami”alisema Mango

IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE




Share it:

habari

Post A Comment: