Kwasababu
kume kuwepo na tuhuma ya wanafunzi wa kike kuwa na mahusiano na walimu shuleni
hadi kupelekea wanafunzi hao kupata ujauzito na wahusika baadhi yao ni walimu kujaribu
kutoa ujauzito huo ili kupoteza ushahidi hali ambayo imesababisha wanafunzi
kupoteza maisha yao na wengine kunusurika kifo, wengine kuacha shule kabisa, na
taarifa hizi zimekuwa zikifichwa kwanzia ngazi ya kijiji,kata na mashuleni
kutokana na wazazi,walezi na baadhi ya
walimu kusaidiana kuficha taarifa hizi .
Aidha
hali hii inayoonekana kukithiri umuhimu wa semina elekezi kwa walimu ambao
pengine wamesahau au hawazijui sheria na kanuni hizo ndiyo maana nimeambatana
na wanasheria kutoka taasisi za umma zilizopo wilayani hapa ili kutoa ufafanuzi
wa sheria hizi jinsi zinavyofanya kazi .
Mkuu
wa Wilaya mhe.Josephat Maganga ameelekeza wakuu wa shule kushirikiana na bodi
ya shule kuandika taarifa ya matukio ya ujauzito yanayotokea katika shule zao
na kuhakikisha zinafika ofisi ya afisa elimu wilaya ambapo ataipeleka ofisi ya
Mkuu wa wilaya, pia walimu wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi ya
Ualimu,
“bahati nzuri nilishawahi kuwa
mwalimu katika chuo cha Ualimu, nikapanda ngazi na kuwa afisa elimu Wilaya
Serengeti,Biharamulo na Chato, kutokana na kufanya kazi kwa kusimamia kanuni na
sheria nikapanda na kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama,
na sasa ni Mkuu wa Wilaya hakika nitaendelea kusimamia na kutekeleza kanuni na
sheria “alisema Maganga.
Alisisitiza
kila mwalimu anawajibu wa kuhakikisha mwanafunzi anayeanza shule anasimamiwa
vizuri mpaka anamaliza shule na walimu kuacha kukaa kimya wanapopata matatizo.
Baada ya semina elekezi Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe mhe. Josephat Maganga ameagiza wakuu wa shule, waratibu elimu kata
kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi, pili walimu kuhakikisha wana
kanuni na sheria, tatu daftari la adhabu shuleni, mwisho wanafunzi wa kike
kuchunguzwa ujauzito kila baada ya miezi mitatu (3) na Maafisa elimu wilaya
kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia utekelezaji wa maagizo hayo.
Imeandaliwa na Afisa habari na Uhusiano Wilaya ya Bukombe Tusa Daniel Mwambenja
Post A Comment: