Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu |
Eneo ambalo liliathiriwa kutokana na kuangukiwa na jiwe likiwa limeshasambaratishwa jiwe hilo na eneo likionekana likiwa wazi kwaajili ya ujenzi wa sehemu hiyo. |
Makamo wa Rais wa Mgodi wa GGM Saimon Shayo akitoa pole kwa wananchi ambae alipatwa na janga la nyumba yake kudondokewa na Jiwe. |
Jiwe likionekana likiwa limetelemka kutoka sehemu liliyokuwa awali na kufika kwenye makazi ya wananchi. |
Wakiangalia maeneo ambayo yanaonekana ni hatari ambayo bado hayajafanyiwa kazi ya kutolewa kwa mawe. |
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum
Mustafa Kijuu ameishukuru kampuni ya Mgodi wa
dhahabu wa Geita (GGM) kwa kutoa msaada wa kuondoa mawe
ambayo yalikuwa na uzito wa tani ishirini
(20) yaliyokuwa yamedondoka kwenye
makazi ya watu.
Hayo ameyasema
baada ya kukutana na viongozi hao katika ofisi yake ambapo walifika kujua shughuli hiyo imeendaje kwa awamu ya kwanza
kabla ya awamu ya pili.
Mh Kijuu
amesema kuwa tetemeko la ardhi lilipotokea mawe mengi yalitikiswa na yaliweza kuvamia maeneo ya makazi ya wananchi na kuharibu majengo na
miundombinu kutokana na ugumu wa
kuyatoa, ndipo mkoa ukaona kuna uhitaji wa kuomba msaada kutoka GGM ili walau mawe
hayo yaweze kuondolewa kwa utaratibu ambao
ni mzuri usioweza kuathiri
wananchi.
“Kiukweli tungekuwa ni sisi wenyewe tusingeweza
kutokana na tani kubwa ya mawe hayo kiukweli tunawashukuru sana Mgodi wa
dhahabu wa Geita kwa kujitolea kuleta mkandarasi ambae amefanya shughuli ya
kutoa mawe hayo maeneo ya makazi ya watu kwani yasingetolewa natambua
yawezekana kuna athari zingejitokeza kwa yale maeneo ambayo yalikuwa
hayajaathirika”Alisema Kijuu.
Makamo wa
Rais wa mgodi wa GGM ,Saimon Shayo,ameelezea kuwa wao kutokana na kwamba ni
majirani kwani Kagera na Geita ni mikoa ipo jirani hali hiyo imewagusa na
kuamua kutoa mchango wa kuondoa mawe hayo ambapo kiasi cha sh,milioni mia moja
na kumi (110) zimetumika kwa awamu ya kwanza kutoa baadhi yam awe yaliyokuwa
yameangukia kwenye makazi ya watu.
Wananchi
ambao walikuwa wameangukiwa na mawe
katika maeneo yao wameishukuru kampuni ya GGM pamoja na mkuu wa Mkoa kwa kuweza
kutoa msaada wa kuondoa mawe hayo kwani endapo wangeachiwa wasingeweza kutokana na uwezo wao wa kimaisha
kuwa chini.
Imeandaliwa na Madukaonline.
Post A Comment: