Meneja wa Manchester United Jose Mourinho |
Shirikisho la Soka nchini England (FA) limemwandikia barua Meneja wa
Manchester United Jose Mourinho likimtaka ajieleze kuhusu matamshi yake juu ya
mwamuzi Anthony Taylor ambaye Jumatatu alichezesha pambano la Liverpool na Man
United huko Anfield na timu hizo kutoka sare ya bila kufungana.
FA imempa Mourinho muda hadi Ijumaa kujieleza na
uamuzi huo wa FA umekuja baada ya shirikisho hilo kuona amevunja Sheria kwa
kuongea kuhusu waamuzi kabla ya mechi wanayopangiwa.
Mara baada yamwamuzi Taylor, 37, kuteuliwa kuchezesha
pambano hio kuliibuka malalamiko, na hasa Mashabiki wa Liverpool, ambao
walilivalia njuga suala hilo kupitia kwenye Mitandao ya Kijamii.
Akiongea na Wanahabari kabla ya Mechi hiyo, Mourinho
aliulizwa kuhusu uteuzi wa Refa huyo na yeye kujibu kwamba “Nadhani Bwana
Taylor ni Refa mzuri sana lakini anapewa presha kubwa na itakuwa ngumu kwake
kuwa na kiwango kizuri cha kuchezesha.”
FA sasa inataka maelezo kutoka kwa Mourinho kwa
kuvunja Sheria iliyotungwa Mwaka 2009 inayokataza mameneja kuongea lolote
kuhusu marefa kabla ya Mechi.
Meneja wa kwanza kabisa
kuadhibiwa na Sheria hiyo alikuwa ni meneja wa zamani wa Man United, Sir Alex
Ferguson, ambaye alishitakiwa Mei 2011 kwa kutoa kauli kuhusu Refa Howard Webb
ambayo haikuwa mbaya bali ilikuwa ya kumsifia pale aliposema alikuwa ni refa
bora zaidi huko England.
Post A Comment: