Kikundi cha Utamaduni cha
Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia
Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo
Oktoba 08,2016.
|
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye amewashauri vijana kutumia
ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.
Ametoa ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga
Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana
kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho
kitawasaidia kupata kipato na kuendesha maisha yao.
“Ngoma za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi
kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza
ajira na kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.
Aidha kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana
kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo
zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani kwa sasa.
“Nawashauri vijana wa kitanzania kuangalia na upande
huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi tupo pamoja nao na
tutawapa ushirikiano ili wafikie
malengo” alisema Mhe. Tulia.
Tamasha hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia
Ackson linafanyika kwa siku mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili
vipatavyo 62 kutoka mkoani Mbeya.
Post A Comment: