NYOTA WA INJILI MMAREKANI APACHIKWA JINA KWA KUPENDA KUKAA AFRIKA YA KUSINI

Share it:










Kati ya waimbaji wa injili nchini Marekani ambaye anaongoza kwa kutembelea Afrika ya kusini mara kwa mara basi mwanakaka VaShawn Mitchell anaongoza, kiasi cha kubatizwa jina la kizulu kutoka kwa marafiki zake wa karibu nchini humo.

Mitchell aliyetamba na wimbo wa 'No body is greater than you' amekuwa akitembelea nchini Afrika 

ya kusini kila mara ambapo aliamua kurekodi DVD mpya hukohuko na hivi karibuni alizindua DVD hiyo aliyoipa jina la 'Secret Place'. Kutokana na kutembelea sana nchini humo hivi karibuni alipotembelea eneo la Soweto alipewa jina la kizulu 'Bhek'Umuzi' lenye maana ya kubwa ya mtu mkubwa ama kiongozi.

Mara baada ya kuweka hadharani jina lake hilo baadhi ya waimbaji wa Afrika ya kusini walionekana kufurahia jina hilo huku kwa upande wa waimbaji wenzake na marafiki nchini Marekani walimtania wakimwambia asijisahau huko nchini Afrika ya kusini anatakiwa kurudi nyumbani kwao Marekani, utani ambao ulimchekesha mwimbaji huyo. Mitchell licha ya kuimba na kujitwalia tuzo mbalimbali pia ni mtunzi mzuri wa nyimbo za injili.
Baadhi ya waimbaji wengine wanaopenda kutembelea nchini Afrika ya kusini ambako hupata mwaliko wa kihuduma ni pamoja Kirk Franklin ambaye wakati wa kifo cha Mandela alikuwa nchini humo na kufanikiwa kuimba katika ibada maalumu ya kumuaga mzee Madiba, wengine ni Israel Houghton, James Fortune, Donnie McClurikin ambaye kwasasa yupo njiani kurudi Johannesburg ambako atakuwa na tamasha mwezi huu na waimbaji wa nchini humo. 

Share it:

mastaa

Post A Comment: