DC KAPUFI AFUTA VIBALI VYA WAGANGA WA JADI

Share it:


Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisistiza kufuta vibali vya                         waganga wa tiba za jadi katika kijiji cha isulwabutundwe

Wananchi wakifatilia maagizo ya mkuu wa wilaya wakati wa mkutano wa hadhara kijiji hapo.


Mkuu wa wilaya akiandika baadhi ya hoja za wananchi juu ya hatua ya  kufutwa kwa vibali vya waganga wa jadi.

Serikali Wilaya ya Geita  imefuta vibali vyote vya waganga wa jadi kutokana na baadhi ya waganga wameendelea kuwa  chanzo cha mauaji ya binadamu na kujenga hofu kwa wananchi kutokana na kuwepo kwa baadhi yao kuendelea na maswala ya ramli chonganishi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl.Herman Kapufi wakati  alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji na kata ya isulwabutundwe wilayani humo ambapo amesema kuwa baada ya kufutwa kwa vibali hivyo,usajili utafanyika upya

Mwl.Kapufi ameeendelea kufafanua kuwa waganga wa jadi wamelalamikiwa kuwa chanzo cha mauaji kwa kuwahamasisha wahalifu kutumia dawa katika kutekeleza uhalifu kuwa kinga ya kutokamatwa.

“Leo nimeandika barua kwa halmashauri zote mbili nimefuta vibali vyote vya waganga wa jadi kuanzia leo mtazipata barua na utaratibu wa kuvipata vibali paka utoke jasho namna gani unakwenda wilayani kwa mganga mkuu wa wilaya unachukua fomu unajaza ukileta ile fomu unapeleka kwenye serikali ya kijiji inakujadili kuwa umeweza kumtibu nani na nani amepona”alisema Kapufi

Kutokana na tamko hilo la serikali,Baadhi ya wananchi wameunga Mkono agizo hilo huku wengine wakiomba kufutwa kabisa shughuli ya waganga wa kienyeji kwani ndio chanzo cha mauaji ambayo yameendelea kujitokeza na kugharimu maisha ya wananchi wasio na hatia



Hatua ya kufutwa kwa vibali vya waganga wa kienyeji imetokana na mauaji  wazee,watu wenye ulemavu wa ngozi na walinzi ambayo yameendelea kutokea wilayani humo.

Imeandaliwa na Madukaonline

Share it:

Darasa huru

habari

Post A Comment: