Baadhi ya wananchi waliofika eneo ulipo mti huo wa maajabu wakistaajabia maajabu ya mwenyezi Mungu huku wengine wakikata mizizi na magome ya mti huo. |
Hata kama mtu hujui matumizi na maana ya mti huo wewe beba utajua mbele ya safari.
Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa mtaa wa samina kata ya
mtakuja wilaya na Mkoa wa Geita
wamejikuta wakiingiwa na taaruki ni baada ya mti mbwa ulionguka kwa kipindi cha miaka mitano
iliyopita kukuta umesimama wenyewe.
MADUKAONLINE imefika katika eneo la Tukio hilo leo majira ya saa
tano asubuhi na kukuta mamia ya wananchi
kutoka katika Mkoa wa Geita na Viunga vyake wakiwa wanachimba mizizi ya mti huo
pamoja na kuchukua magome yake kwa madai ya kwenda kuomba matatizo yao.
wananchi waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kuwa mti huo ulianguka tangu mwaka 2011 na jana majira
ya saa sita mchana walipata habari kuwa mti huo umesimama
Mwenyekiti wa mtaa huo John Barenge pamoja na mzawa mmoja Abudara
wamesema sehemu hiyo wazee wa zamani walikuwa wanaitumia kwa ajili ya matambiko
kwa kutibu watu.
Diwani wa kata ya mtakuja
Constatine Molandi amewataka wananchi wake kutotumia mizizi na magome ya mti huo kwa ajili ya kunywa kwani hakuna
anayejua madhara ambayo yanaweza kujitokeza .
Baadhi ya wazee ambao awakutaka kuchukuliwa sauti zao wala kuandikwa majina yao wamesema kuwa mambo
haya yanaanza kutokea kwa sababu imeandikwa kwenye vitabu vya mungu.
Post A Comment: