Mwenyekiti ambaye amemaliza muda wake kwenye mtaa huo,Joel Mazemule akielezea namna ambavyo wananchi hao walivyoshauliwa kupisha maeneo hayo
Wananchi wa mtaa wa
kabahelele Kata ya katoro wamepewa siku
saba kupisha maeneo ambayo wameingia kwenye kituo cha afya hali ambayo
imepelekea kuwepo kwa stofahamu huku wengine
wakibubujikwa na machozi ,baada ya mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi
kutoa agizo hilo.
Kaya ambazo zinatarajia kubomolewa katika zoezi la
kupisha eneo hilo ambalo lilivamiwa kinyume na utaratibu ni zaidi ya 28 zenye
wakazi takribani 128
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa
amri ya wananchi hao kuondoka baada ya serikali kubaini wanaishi ndani ya eneo
la Kituo cha Afya Katoro na kwamba zoezi la kubomoa nyumba zao litaanza
kutekelezwa Januari 11 siku ya Jumatano ikiwa ni maandalizi ya kujenga uzio na
chumba cha kuhifadhia maiti.
Wakizungumza kwa uchungu
mbele ya Mkuu wa Wilaya na katika eneo
hilo wakazi wa eneo hilo Paulina Mtabazi, Stanley Mwigaya, pamoja na Paulo
Magala wamesema wamekuwemo ndani ya eneo
hilo kwa muda mrefu, huku wengine wakidai waliuziwa na viongozi wa vijiji.
Pamoja na maelezo hayo
msimamo wa Mkuu wa Wilaya ukawa ni wananchi kupisha maeneo hayo kabla ya
jumatano ya wiki ijayo, huku akipinga hoja za
kuongoza muda na kwamba ikifika siku hiyo kikosi cha kutuliza Ghasia FFU
kitatia nanga eneo hilo ili kuimalisha ulizi wakati wa zoezi la kubomoa nyumba.
“Mimi sitoi muda leo
ninapondoka wewe tafuta mafundi chukua
vitu vyako mbao zako,bati zako na kila kitu nimeongeza siku moja tu jumatano
asubuhi FFU na mimi nakuja hapa na siku ya jumanne vifaa vya kubomolea
vitakuwepo maeneo haya”alisisitiza Kapufi
Madukaonline imezungumza na mwenyekiti aliyemaliza muda
wake Joel Mazemule ambapo amekili kuwa eneo ambalo wananchi wanalilia ni mali
ya serikali na kwamba walishawai kuwaambia wananchi hao kuwa ni vyema wakapisha
kwani muda wowote watakuja kutolewa.
“Wakati mimi nikiwa ni
mwenyekiti nilishawai kuwaambia kwamba siku yoyote iwe miaka kumi ishirini
lazima eneo hilo serikali itakuja kulichukua maana ni mali yake na sio mali yao
tatizo ambalo limewaponza wananchi ni kumsikiliza diwani aliyemaliza muda wake
Mama Mingisi alikuwa anawaambia wasiwe na wasi wasi matokeo yake ndio hayo
ambayo leo yamewakuta”alisema Mazemule
Hata hivyo maamuzi haya
yanakuja siku chache baada ya waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
serikali za mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene kuagiza eneo la kituo cha Afya
lizungushiwe uzio, huku akitaka agizo la Waziri Mkuu kupanuliwa kwa Kituo cha
Afya Katoro litekelezwe haraka iwezekanavyo.
|
Post A Comment: