Mtambo unaopeleka hewa ukiangaliwa kwa makini.
NI SIKU ya pili
sasa tangu wachimbaji kumi na nne (14) ambapo simanzi, masikitiko yameendelea kutanda
baina ya jamii na ndugu wa wachimbaji ambao wamefukiwa na udogo kwenye Mgodi wa RZ uliopo Kijiji cha Nyarugusu
Wilaya ya Geita hata hivyo jitihada na zoezi la kuwaokoa bado linaendelea .
Zoezi la uokoaji linalosimamiwa na kamati ya ulinzi na
usalama ya Mkoa, Ofisi ya Madini Kanda ya ziwa magharibi ikiyashirikisha
makampuni ya Migodi ikiwemo GGM na Busolwa
mine, imeelezwa hatua iliyofikiwa hadi leo saa 1:30 asubuhi walikuwa wamechimba takribani mita 20 kati ya
30 ili kuwafikia wachimbaji hao.
Kufuatia hatua
hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
aliwataka ndugu na jamaa wa watu 14 waliofukiwa
na kifusi ndani ya Mgodi wa RZ kuwa na
subira wakati waokoaji wakiendelea na Zoezi hilo.
“Mimi niwatake
ndugu na jamaa kuendelea kuvuta subira wakati waokoaji wakiendelea na kutumia mashine kwa ajili ya kuwaokoa watu
waliozama chini ya Mgodi huo jambo ambalo hata Mkoa wa Geita umelipokea kwa
masikitiko makubwa sana,’’alisema Kyunga.
Aidha Mkuu huyo
wa Mkoa ametoa kalipio kali kwa
wawekezaji ambao hawajali ustawi wa wafanyakazi wake kwa uzembe ambao unaweza
kuepukika na kwamba alisikitishwa sana namna mgodi wa RZ ambavyo ulikuwa
haujali masuala ya miundombinu yake.
ZOEZI la uokoaji limeendelea huku matumaini ya wengi
yakizidi kupotea kutokana na ugumu wa kazi dalili hata kidogo hazionekani
lakini kamishina wa madini kanda ya ziwa magharibi Bw. Yahaya Samamba amesema zoezi
hilo litakamilika na watu watakuwa salama kutokana na hewa wanayoipata kupitia
mpira unaoingiza kwa kutumia mashine.
Maduka online usiku kucha imeshuhudia hatua kwa hatua
zoezi hilo, licha ya baadhi ya maafisa wa serikali wakishindwa kuvumilia
kukesha kwenye zoezi hilo.
Kamishina
msaidizi wa madini kanda ya Ziwa Yahaya Samamba ameendelea kuelezea kuwa pamoja na kuunda kamati ya uokoji wamekutana
na changamoto kubwa kwa sababu ya duara walikozama watu hao kuwa chini ya
kilomita 35.huku akisema wanaendelea kuomba mashine nyingine kutoka kwa
makampuni mengine kama zoezi litaonekana kuwa na ugumu.
“Tumeunda
kamati ya uokoji na kamati yetu imehusisha makampuni yote yalioleta mashine zao
kwa ajili ya uokoaji huo huku naye akiwataka wananchi kutoanza kutoa lawama kwa
baadhi ya vyombo vya Serikali na ngazi nyingine kwenye wizara ya madini,,
alisema Samamba.
Maduka online ilibahatika kukutana uso kwa uso na diwani wa
kata ya Nyarugusu yalipo maafa hayo, Swalehe Juma alisema janga hilo limemnyima usingizi na kwamba
siku ya jana alilazimika kukesha na waokoaji.
“Mwandishi
nakushukuru kwa kuwa nasi kwenye zoezi hili ni kweli mimi nyumbani ni karibu
hata kwa miguu naweza kutembea nikafika lakini siwezi kwenda jambo hili
limeninyima raha nitawezaje kwenda kwangu wananchi wangu wako ndani ya
shimo,’’alisema Juma.
Hata hivyo
baadhi ya wananchi waliohudhuria kushuhudia tukio hili la aina yake katika
wilaya ya Geita ikiwa ni mwanzoni mwa mwaka wa 2017, walisema lawama kubwa
wanazielekeza kwa mamlaka za madini kwa kushindwa kujisimamia katika
kuhakikisha uchimbaji ulio imara kwenye migodi unaboreshwa.
“kaka hili
jambo linasikitisha sana hebu fikiria tangu usiku wa tarehe 26 saa saba usiku
mpaka leo siku nyingine ya tarehe 27 tumekutana tena watu wako ndani ya kifusi
je watapona licha ya matumaini tunayopewa…Mimi hapa naelekeza lawama kwa ofisi
ya Madini Mkoa wa Geita hawakagui migodi ipasavyo,’’alisema Mkazi wa Nyarugusu
Saidi Mrisho.
“Kwanza
nashangaa nilimsikia jana kamishina wa madini kanda ya ziwa akisema chanzo ni
kutokana na miti iliyokuwa imeshikilia ukuta kuwa imeoza sasa hapa najiuliza
je, kazi ya ofisi ya madini nini wanakagua nini na je waliwahi kuwaambia kuwa
miti hii haifai katika ukaguzi wao
inapaswa serikali nayo iwachukulie hatua kubwa kwa uzembe huu
haiwezekani,’’alisisitiza.
Katika shughuli
za uokoaji wananchi hawakuacha kuipongeza kampuni ya uchimbaji wa madini ya
Busolwa Mine inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Baraka kwa kujitolea mashine zake
za greda kuhakikisha wanafanikisha adhima ya kuwaokoa watanzania 13 pamoja na
raia wa china Bw. Meng Juping, ambaye anadaiwa hakuwa na redio koll kama
ilivyokuwa kawaida yake wakati anakwenda kutekeleza majukumu yake ya uzalishaji
wa madini ya dhahabu.
Hata hivyo Madukaonline ilishuhudia kikosi cha zima
moto na uokoaji Mkoa wa Geita pamoja na jeshi la polisi wakiendelea na majukumu
yao ya kuhakikisha eneo hilo liko salama.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: