Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akielezea dhamira ya dhati ya kuendelea kuchochea maendeleo katika wilaya ambayo anaisimamia kwa sasa.
Chama
cha mapinduzi ccm wilaya ya Geita kimeadhimisha miaka arobaini (40)tangu
kuanzishwa kwake mnamo Februari,mwaka
1977 kwa kufanya shughuli ya ujenzi wa kituo cha afya kwenye kata ya
shiloleli iliyopo halmashauri ya mji wa Geita.
Akizungumza
na wananchi kwenye shughuli hiyo ya ujenzi wa kituo cha afya Mwenyekiti wa ccm wilayani
humo,Barnabas Mapande,amemwambia mhandisi kusimamia kwa umakini ujenzi wa boma lisije
kutokea tatizo baada ya kuwa umemalizika ujenzi
“Najua
wananchi wanatumia nguvu nyingi kwenye ujenzi huu ambao wamejitolea kwa dhati
sasa nakuomba Mhandisi wa ujenzi
kusimamia kwa umakini ujenzi huu ili isije ikatokea tena kuonekana kwamba
majengo yamejengwa chini ya kiwango”Alisisitiza Mapande.
Diwani
wa kata ya Shiloleli,Bonface Kaswahili Wapihatenabei ameelezea pamoja na ujenzi
huo kuendelea bado wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa maji ya kujengea
kituo hicho cha afya.
“Pamoja
na kwamba ujenzi huu unaendelea lakini changamoto kubwa ni upungufu wa maji ya
kutosha pamoja na kwamba Mkurugenzi wetu wa halmashauri ya mji ametusaidia
visima sita lakini havitoshelezi kwa mahitaji yaliyopo”Alisema Kaswahili
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi ambao wamezungumza na maduka online ,wameeleza
kuwa kukamilika ujenzi wa kituo hicho cha afya kutarahisisha safari ya muda
mrefu kutembea umbali mrefu kufuta huduma
ya afya huku wakina mama wajawazito kujifungulia njiani.
Aidha
Katibu mwenezi wa chama hicho,Jonathani
Masele,ameeleza kuwa chama hicho kitaendelea kujitolea kwa shughuli za kimaendeleo
kwa wananchi ili kufuata ilani ya
uchaguzi ya mwaka 2015.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
Post A Comment: