Mkuu wa mkoa wa Geita,Meja Jenerali Ezekiel Kyunga,akitfungua kikao cha wadau wa pamba Mkoani Humo. |
Wajumbe wakifatilia kwa makini kikao Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Bukombe Nicas Mayala |
Wajumbe wakiendelea na majadiliano |
Wakuu wa wilaya Mkoani Geita wakifatilia kikao. |
Afisa kilimo wilaya ya Bukombe Joseph Machibya akitoa maelezo namna ambavyo wameweza kupiga hatua kwenye kilimo cha pamba. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisikiliza kwa makini kile ambacho kilikuwa kinatolewa na mkuu wa mkoa wa Geita. |
Serikali
mkoani Geita ,imesema kuwa itahakikisha inaboresha zao la pamba kwa kutumia
viadudu ambavyo vitasaidia kunusuru pamba kwenye maeneo ya vijijini
ambako wakulima wengi wanaendelea kulima.
Akizungumza
kwenye kikao cha wadau wa zao la Pamba kilichofanyika katika ukumbi wa
Mkutano wa Mkoa na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Wilaya
zote za mkoa wa Geita wakiwemo Maafisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika pamoja
na Wakuu wa Bodi ya Pamba kanda ya ziwa,
Mkuu
wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,amesema kuwa pamoja
na hali ya changamoto ya ukame na mvua
kunyesha kwa uchache bado wakulima wameitikia wito na kulima hali
ambayo kwa sasa inatia matumaini kutokana na pamba kuoto vizuri vijijini.
“Huko
vijijini wamaenza kulalamika kutokana na upungufu wa viuadudu sasa na sisi hapa
lazima tupate uvumbuzi kwamba hili tatizo la viuadudu tunalipatia majibu sahihi
ambayo yatawasaidia wakulima wetu kule vijijini, wakulima wameitikia vizuri
pamoja na hali hii ya mvua ambazo sio kamilifu, mvua ni chache, mvua ni haba
lakini wakulima wameitikia” alibainisha mh kyunga
Kwa
upande wao baadhi ya wajumbe akiwemo Emily Kasagara Mkuu wa Idara ya
Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Geita na Safari Mayala Mwenyekiti wa halmashauri
ya Wilaya ya Bukombe wameelezea changamoto dhidi ya zao la pamba na kusema kuwa.
“Kuna
changamoto mbalimbali zilizojitokeza kuhusiana na zao hli la pamba, moja ni
kuwa wakulima wengi walielekeza nguvu zaidi kwenye mazao ya chakula kipindi
mvua zilipoanza kunyesha na badala ya zao la pamba kwa hiyo ndio maana hata
katika taarifa yetu kile kilimo cha pamba kiliextend mpaka mwezi Januari kwa
sababu mvua zilipoanza kunyesha tu wakawa wamerash kulima mazao ya chakula
lakini baadae sasa wakalima zao letu la pamba ambalo limeenda mpaka Januari” alisema
Aidha
katika msimu wa mwaka 2016-2017 Mkoa
ulilenga kulima jumla ya tani elfu sitini na saba na mbili (67,002) zilizotarajiwa
kutoa mavuno ya tani elfu tisini na tatu mia nne thelathini na saba (93,437) lakini changamoto ya mvua za vuli kutonyesha vizuri katika
baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Geita imeweza kusababisha malengo hayo
kutokufikiwa.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: