|
Mwenyekiti wa Bodi NHIF na Spika mstaafu wa Bunge mama Anna Makinda akisisitiza juu ya huduma kuboreshwa katika mfuko wa Bima ya afya wa Taifa. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa na mwenyekiti wa Bodi ya NIHF wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mkoa wa Geita juu ya mfuko wa bima ya afya . |
|
Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu na Mbunge wa Jimbo la Busanda Lorencia Bukwimba wakifatilia mkutano . |
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima wa Taifa Mkoani Humo. |
|
Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu,akielezea namna ambavyo kumekuwepo na changamoto za huduma ya afya katika jimbo ambalo analiongoza. |
|
Mbunge wa Bukombe Dotto Biteko akichangia swala la huduma ambazo zinatolewa na mfuko wa Bima ya afya wa NHIF. |
|
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF. |
|
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Angela Mziray akifafanua namna ambavyo NHIF imekuwa ikisaidia wa gonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza. |
|
Meneja wa NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya akielezea namna ambavyo shughuli zimekuwa zikifanyika Mkoani Geita za kuandikisha wanachama wapya. |
|
Wajumbe wakiendelea kufatilia mkutano. |
|
Mwenyekiti wa Bodi NHIF na Spika mstaafu wa Bunge mama Anna Makinda,akiwashkuru wajumbe ambao wameuzulia Mkutano huo. |
|
Picha ya pamoja mwenyekiti wa Bodi ya NHIF pamoja na wajumbe ambao wameshiriki mkutano huo. |
Kutokana na kuwepo kwa baadhi ya vituo vya afya kuwa na mazingira yasiyo mazuri ya kimiundombinu na lugha chafu kwa baadhi ya hudumu wa afya,ukosefu wa dawa na upungufu wa wataalam imeelezwa kuwa chanzo ambacho kimekuwa kikisababisha juhudi za wananchi kutokujiunga na mfuko wa Bima ya afya .
Akizungumza katika mkutano wa wadau wa afya Mkoani Geita mwenyekiti wa Bodi NHIF na spika mstaafu wa Bunge Anna Makinda amesema wanafanya maboresho ya kuhakikisha kila atakayejiunga awe na uwezo wa kupata huduma kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoani hivyo watumishi wachache wasiharibu fursa ya wananchi kupata huduma nzuri.
“Inatakiwa mtu ambaye anakata NHIF aende akatibiwe kwenye ngazi ya zote ndani ya Mkoa sio haishie kwenye zahanati ,zahanati zingine zimekuwa zikikatisha tama unakuta mganga hayupo hata dawa hazipo jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa wananchi ninachokisema wakurugenzi zungumzeni na wananchi harafu tushirikiane katika mambo yafatayo lazima dawa ziwepo kituo cha afya kiwe kituo cha afya kweli Mganga mkuu nadhani yupo hakikisha unafatilia haya mambo kwa umakini zaidi”Alisema Mama Makinda
Hata hivyo kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa NHIF Angela Mziray ameongezea kuwa Bado wananchi wanakabiliwa na magonjwa ambayo elimu hawana na ukiangalia mfuko unaingia gharama ya asilimia 19 kutibu magonjwa yasiyoambukiza.
“Kutokana na mtinda wa maisha ambayo tumekuwa tukiishi kila siku unajikuta magonjwa ya siyoambukizwa yamekuwa yanaongezeka kwa kiasi kikubwa sana sasa kutokana na hili mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya iliona ni vyema ukaboresha kwa kughalamia asilimia 19 za matibabu kwa mgonjwa” Alifafanua Mziray.
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amewasisitiza watumishi wa sekta ya afya kuakikisha wanakuwa na maadili ya kazi zao na kuachana na tabia ya ambazo zimekuwa zikiwakatisha tamaa wagonjwa.
“Inatakiwa watumishi katika vituo kujirekebisha na kuzingatia taratibu za kuadirifu kamavile walivyoelekeza baada ya kuwa wameitimu mafunzo kuwa watafanya kazi kwa uadilifu na pindi wanapofika kwenye vituowamekuwa wakichukua tabia ambazo sio nzuri kwa wateja nah ii ni kutokana na majibu ambayo wamekuwa wakipatiwa wateja sio mazuri”Alisisitiza Kyunga
Pamoja na serikali kusisitiza swala la watanzania kutumia bima za afya bado tatizo ni kubwa kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu hivyo mamlaka husika zimetakiwa kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa mfuko wa Bima ya afya.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: