Mkuu wa
Mkoani wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,amewaagiza
wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanasimamia vyakula vilivyopo ikiwan ni
pamoja na kudhibiti uhuzwaji wa nafaka kwenye wilaya na mikoa jirani.
Mh,Kyunga
ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea maghala ya vyakula
kwenye wilaya za Geita,Bukombe na Mbongwe lengo likiwa ni kujionea hali ya
chakula Mkoani humo
Amesema
kuwa ni vyema kwa wakuu wa wilaya kudhibiti chakula kilichopo ikiwa ni
pamoja na kuwaelekeza wananchi kutunza mazao katika kipindi hiki ambacho mvua
zimekuwa ni za kusuasua
“Niwaombe
wakuu wa wilaya zote kuwa waangalifu na kukilinda chakula kilichopo ili Wilaya
na Mikoa ya jirani isije ikachukua na kutuacha hatuna tena chakula lazima hiki
kilichopo kitunze na kuhifadhiwa na muwahimize wananchi walime mazaa ambayo
yanakubaliana na mvua kidogo Mfano,Viazi Mtama na muhogo”Alisema Kyunga
Akisoma
taarifa ya mazao na hali ilivyo kwasasa kwenye soko la kibiashara Katibu wa
wafanya Biashara Soko la ccm Kata ya Katoro,Charles Mlale alisema kuwa Bei ya nafaka kwa mwaka huu imepanda
zaidi ikilinganishwa na mwaka jana kwani mwaka jana gunia la mahindi walikuwa
wanachukulia kiasi cha sh elfu themanini kwa sasa imefika kiasi cha laki na
ishirini
Akizungumza
kwa niaba ya wakuu wa wilaya ,Mkuu wa wilaya ya Bukombe Josephat Maganga
amemwakikishia Mkuu wa Mkoa kufanyia kazi maagizo aliyoyatoa ikiwa ni pamoja na
kuakikisha hakuna mtu ambaye hatatoka mikoa ya jirani au wilaya kuja kununua
mazao yaliyopo kwenye wilaya wanazozisimamia .
Post A Comment: