Mwalimu Medard Zacharia aliyevamiwa na kupigwa na wazazi baada ya kutoa adhabu kwa mwanafunzi ambaye alizimia shuleni Hapo |
Mwalimu Deogras Ristone akielezea masikitiko yake kutokana na kupigwa na wazazi kwenye shule ambayo wanafundishia |
Baraza la shule likijadili na kuweka maadhimio ya kutokufundisha hadi pale wananchi ambao wametenda kitendo cha kuwapiga walimu watakapochukuliwa hatua za kisheria. |
Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Geita,Mwalimu John Kifimbi akielezea kusikitishwa kwake juu ya kitendo ambacho kimefanywa na wananchi. |
Walimu wawili wa shule ya Msingi
Isabilo kata ya Bugurula wilaya na Mkoa
wa Geita wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa fimbo na wananchi waliovamia
shule hiyo kulipiza kisasi baada ya walimu hao kudaiwa kutoa adhabu ya viboko
kwa mwanafunzi mmoja aliyepandisha mapepo.
Tukio la kushambuliwa kwa walimu
hao limetokea Januari 25,mwaka huu na kwamba walimu 10 wa shule hiyo wamegoma
kuingia madarasani kufundisha wakiomba serikali iwahamishe kutoka shuleni hapo
kwa kuwa wamefedheheshwa na wananchi.
Walimu walishambuliwa ni Medard Zacharia
na Deograsi Ristone ambao wanamajeraha
sehemu mbalimbali za miili Wakizungumza na madukai online kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kitendo walichofanyiwa sio cha
uungwana na kwamba muda mwingine wanakosa amani wanapokumbuka tukio hilo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Athuman Augustine anasema Chanzo cha tukio hilo ni walimu kutoa adhabu ya viboko vitatu vitatu kwa kila mwanafunzi ambaye hakwenda kufanya zamu ya usafi wakati wa likizo na ndipo wakati wa utekelezaji wa adhabu hiyo mmoja wa wanafunzi waliopewa adhabu alipandisha mashetani.
“Wakati wa kutoa adhabu mtoto mmoja anayedhaniwa kuwa na mapepo,alianguka na kuzimia hali iliyoamsha gadhabu kwa wazazi na kusababisha wananchi kuivamia shule na kuanza kuwashambulia walimu kwa fimbo”Alisema Athuman.
Mwl,Medard Zakaria,ameeleza kuwa yeye alitoa adhabu hiyo
kama mwalimu ambaye alikuwa dhamu siku hiyo .
“Nilitoa adhabu kama mwalimu ambaye nilikuwa zamu lakini nashangaa cha kusikitisha wakati nawaachi wanafunzi mmoja wao ambaye jina limehifadhiwa alianguka akiwa darasani na kuanza kupiga kelele kutokana na hali hiyo sisi kama walimu tulikwenda kumtazama lakini hali yake haikuwa njema ilituradhimu kupiga simu Hospital ya Nzera kuomba msaada wa kuja kuchukuliwa wakati tulipokuwa tunaendelea na jitihada hizo ndipo kundi la wazazi likafika likiwa na asira wakiuliza kwanini umewapiga watoto wetu sikujibu kitu kutokana na hilo moja kati ya wazazi alinivamia na kuanza kunichapa fimbp mbele ya wanafunzi uku akiniuliza ni kwanini unawapiga wanafunzi ndio hali ilivyokuwa”alisema Zakaria
Mwalimu Deogras Ristone,ameiomba serikali kupitia kwa afisa elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya kuwahamisha sehemu hiyo kwani kwasasa awana amani ya kuendelea kufundisha wala kufanya kazi kwenye mazingira ambayo wamefanyiwa kitendo cha kudhalilishwa mbele ya wanafunzi ambao wanawafundisha .
Kaimu mkuu wa shule ya msingi
Isabilo Mwl.Athuman Augustine amesema sababu ya kuadhibiwa kwa wanafunzi ni
kutokana na kutokufika shuleni hali ambayo iliwapelekea kuwapa adhabu ya viboko
vitatu kwa kila mwanafunzi ambaye hakuhudhuria siku ya usafi shuleni wakati wa
rikizo
Katibu wa chama cha walimu Wilayani Geita,John Kafimbi amefafanua kuwa
swala hilo alitavumiliwa kuona walimu wanadhalilishwa na kwamba ni vyema kwa serikali ikachukula hatua kali ambazo zitawasaidia walimu hao kwani vitendo vya
namna hiyo vimekuwa vya muda mrefu na hakuna hatua zinazochukuliwa.
“Kwakeli tunasikitika sana kuona bado kunauonevu mkubwa kwa walimu sisi kama chama cha walimu tupo kwaajili ya kuwatetea walimu wote na kwamba haya hayawezi kuvumilika haiwezekani mwananchi anatoka nyumbani anakuja kumpiga mwalimu shuleni uonevu huu kiukweli ni Mkubwa na kamwe hatutakaa kimya naomba serikali ilione hili na hatua zichukuliwe kwa wote ambao wametenda unyama wa namna hii zamani walimu walikuwa wanavyamiwa wakitoka Benki na hatujawai kuona hatua zikichukuliwa namwomba Mkurugenzi hatoe uamishwa kwa walimu hawa.”alisisitiza Kafimbi
Afisa mtendaji wa kijiji hicho,Bi Sophia Wiliam amewapa pole walimu hao na kuhaidi kuwa swala hilo la kupigwa kwa walimu litashughulikiwa na wahusika watachukuliwa hatua kwa kuwa kitendo hicho kinadhalilisha kada ya ualimu.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Post A Comment: